-
Salehi: Waandishi wa habari wa kigeni 600 kuripoti mazishi ya Ayatullah Khamenei
Jul 02, 2026 11:49Abbas Salehi Waziri wa Utamaduni na Miongozo ya Kiislamu wa Iran amesema kuwa takriban waandishi habari na wawakilishi wa vyombo vya habari 600 kutoka nje ya nchi wataripoti shughuli ya mazishi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, yaliyopangwa kufanyika kuanzia tarehe 4 hadi 9 mwezi huu wa Julai.
-
Zaidi ya nchi 90 zatangaza utayarifu wa kuhudhuria mazishi ya Kiongozi shahidi wa Iran
Jul 02, 2026 03:49Wawakilishi kutoka zaidi ya nchi 90, pamoja na viongozi wa kidini, wasomi na watu mashuhuri kutoka kote duniani, wametangaza utayarifu wao wa kuhudhuria mazishi ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.
-
Iran yaapa kulipiza kisasi 'damu safi ya Kiongozi aliyeuawa shahidi kwa wakati unaofaa'
Jul 02, 2026 03:47Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran limetangaza kuwa wahusika wa uhalifu na mauaji dhidi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei na watu wa Iran watakabiliwa na adhabu "kwa wakati unaofaa" kutoka kwa "viumbe waadilifu," huku nchi hii ikijiandaa kwa mazishi ya Imam Sayyid Ali Khamenei.
-
China: Vikwazo vya upande mmoja dhidi ya Iran vinapaswa kuondolewa haraka iwezekanavyo
Jul 02, 2026 03:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Guo Jiakun, amesisitiza umuhimu wa kuondolewa haraka iwezekanavyo vikwazo vya upande mmoja vilivyowekwa dhidi ya Iran, huku akikaribisha uwezekano wa kuondolewa vikwazo na masharti yaliyowekwa dhidi ya Tehran.
-
Lamerd iligeuzwa vipi kuwa uwanja wa majaribio ya silaha za maangamizi ya umati za Marekani?
Jul 01, 2026 12:02Takriban miezi mitatu imepita tangu kumalizika kwa uvamizi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa kizayuni wa Israel katika ardhi ya Iran, lakini kila siku, na kufuatia kuchapishwa nyaraka mpya na picha pamoja na simulizi tofauti, viwango vipya vya jinai za wavamizi hao vinafichuliwa.
-
Mtaalamu wa Uislamu Kenya: Urithi wa Ayatullah Ali Khamenei katika kusimama kidete utaendelea kuwa dira
Jul 01, 2026 10:24Mtaalamu wa masuala ya Kiislamu kutoka Kenya katika mahojiano na Pars Today: Urithi wa Ayatullah Khamenei unaelekeza mwelekeo wa nchi za Kusini mwa Dunia katika harakati za kulinda heshima na uhuru wao.
-
Pezeshkian na Narendra Modi wasisitiza kuimarisha ushirikiano wa nchi zao
Jul 01, 2026 10:23Rais wa Iran na Waziri Mkuu wa India wamesisitiza azma thabiti ya nchi zao ya kukuza na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili.
-
Qalibaf: Hakutakuwa na mazungumzo mapya na Marekani kabla ya kutekeleza ahadi zake
Jul 01, 2026 10:20Mkuu wa timu ya Iran ya mazungumzo na Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitaingia katika mazungumzo yoyote mapya na Marekani mpaka masharti yote yaliyomo katika hati ya makubaliano ya maelewano iliyopo yatakapotekelezwa kikamilifu.
-
Iran yasafirisha mapipa milioni 50 ya mafuta baada ya kuondolewa vikwazo vya Marekani
Jul 01, 2026 10:17Kufuatia kupunguzwa kwa vikwazo vilivyokuwa vinaikabili sekta ya mafuta, Iran imesafirisha takriban mapipa milioni 50 ya mafuta katika kipindi cha wiki mbili zilizopita, na inakadiriwa kuwa imepata mapato yanayozidi dola bilioni 3.5 za Kimarekani.
-
Mataifa zaidi ya 90 kuwakilishwa katika Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu
Jul 01, 2026 03:41Dunia inashuhudia mshikamano wa kipekee kufuatia taarifa kwamba wawakilishi kutoka nchi zaidi ya 90, pamoja na viongozi wa kidini, wasomi, na watu mashuhuri kutoka kila pembe ya dunia, wanatarajiwa kushiriki katika shughuli za mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.