-
Baghaei: Iran inafuatilia hatua kwa hatua utekelezaji wa Marekani wa MoU
Jul 01, 2026 03:40Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, Tehran itafuatilia, dakika kwa dakika, iwapo Marekani itazingatia makubaliano ya maelewano (MoU) ya kumaliza vita, na akaonya kwamba Jamhuri ya Kiislamu haitatekeleza wajibu wake chini ya makubaliano hayo ikiwa ni upande mmoja pekee unaoyatekeleza.
-
Waziri: Iran itajibu ukiukaji wowote wa usitishaji vita
Jul 01, 2026 03:31Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hakiuna shaka yoyote kwamba, Tehran itajibu kwa nguvu zote ukiukaji wowote ule wa usitishaji vita.
-
Rais Pezeshkian asema Iran itatekeleza mapatano ikiwa Marekani itafanya hivyo
Jun 30, 2026 11:31Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesisitiza kuwa makubaliano yoyote kati ya Iran na Marekani lazima yajikite katika heshima ya pande zote na ahadi za pamoja, na si kwa kutumia vitisho au shinikizo la upande mmoja.
-
Jeshi: Mazishi ya Kiongozi Shahidi yatakuwa mwamko wa kimataifa dhidi ya ugaidi na jinai za Marekani na Uzayuni
Jun 30, 2026 11:23Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limesema kuwa sherehe za kitaifa za kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zitatumika kama jukwaa la harakati za kimataifa za kulaani ugaidi na maandamano hai dhidi ya jinai zinazofanywa na mhimili wa Marekani na Uzayuni.
-
Pezeshkian: Dola bilioni 6 za Iran zinazozuiwa Qatar kuachiliwa
Jun 30, 2026 03:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, ametangaza kuwa kiasi cha dola bilioni 6 mali ya nchi hii zinazozuiliwa Qatar kufuatia mashinikizo ya Marekani, zitaachiliwa.
-
Wasomi wanawake wa Iran wataka Marekani na Israel ziwajibishwe kwa jinai zao
Jun 30, 2026 03:27Kundi la wanazuoni wanawake wa Iran, wasomi wa taaluma mbalimbali na wataalamu wa masuala ya utamaduni, limesambaza barua ya wazi likirekodi ukiukaji wa kimfumo uliofanywa na Marekani na Israel wakati wa vita vya hivi karibuni dhidi ya Iran, na limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura za uwajibikaji.
-
Kinyume na propaganda za adui, sekta ya ulinzi ya Iran inaendelea kupata mafanikio: Naibu Mkuu wa Jeshi
Jun 29, 2026 12:29Kamanda wa Jeshi la Iran amesema Jamhuri ya Kislamu imepata mafanikio endelevu katika teknolojia ya ulinzi wa ndege zisizo na rubani na anga licha ya madai ya uhasama ya vyombo vya habari.
-
Sardasht; Jeraha Lisilosahaulika Duniani
Jun 29, 2026 07:49Julai 28, 1987, imewekwa alama katika kalenda rasmi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama kumbukumbu ya moja ya jinai za kivita za kutisha dhidi ya ubinadamu. Siku hii, inakumbushia shambulio la kikatili la mabomu ya kemikali katika mji wa Sardasht lililofanywa na utawala wa Baath wa Iraq; jinai ambayo ilitekelezwa kwa uungaji mkono na kimya cha aibu cha madola ya Magharibi.
-
Araghchi: Jukumu la kupanga na kusimamia shughuli Mlango-Bahari wa Hormuz ni la Iran
Jun 29, 2026 03:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema kuwa jukumu la kupanga na kusimamia shughuli katika Mlango-Bahari wa Hormuz ni la Iran pekee, akisisitiza kwamba hakuna taasisi wala nchi nyingine yenye mamlaka au wajibu katika suala hilo.
-
Katika ujumbe wa Wiki ya Mahakama, Kiongozi aamuru kufuatiliwa kisheria uhalifu wa kivita wa Marekani na Israel dhidi ya Iran
Jun 28, 2026 13:02Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei ametoa wito kwa Mahakama ya Iran kufuatilia na kurejesha haki za taifa ambazo zimekiukwa kutokana na vita vya uchokozi vya Marekani na Israel tangu mwaka jana.