-
Mkuu wa Usalama: Iran itaendelea kufunga Hormuz hadi Marekani itimize majukumu yake
Aug 23, 2026 14:24Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu itafubaza mashinikizo ya kiuchumi ya Marekani ikiwa ni pamoja na kuzichukulia hatua nchi ambazo zinashiriki katika “vita vya kiuchumi” vya Marekani dhidi ya Iran.
-
Kaimu Waziri wa Ulinzi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitasalimu amri kwa kuwekewa mashinikizo
Aug 23, 2026 03:28Kaimu Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema, taifa hili limeishinda kimkakati Marekani na utawala wa Kizayuni kwa kutegemea uwezo wake wa ndani, na akasisitiza kwamba: Jamhuri ya Kiislamu haitasalimu amri katu kwa kuwekewa mashinikizo.
-
Meja Jenerali Safavi: Jina la Iran linapaswa kuwa jinamizi la daima kwa tawala vamizi
Aug 22, 2026 12:24Mshauri Mkuu wa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Meja Jenerali Sayyed Yahya Rahim Safavi, amesema uzoefu wa Iran katika vita na makabiliano yake na Marekani na utawala wa Israel unaonesha umuhimu wa kuimarisha uwezo wa kiulinzi na kujenga nguvu ya kuzuia uchokozi.
-
Iran yalaani vikwazo vipya vya Marekani na kuvitaja kuwa hujuma dhidi ya mamlaka ya nchi
Aug 22, 2026 12:22Iran imelaani vikali vikwazo vipya vya kiuchumi vilivyotangazwa na Marekani, ikisema hatua hiyo ni ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala nchi huru na jaribio la Washington la kujipa mamlaka juu ya mataifa mengine.
-
Salehi-Amiri: Afrika Kusini ni lango la Iran kuingia katika soko la utalii barani Afrika
Aug 22, 2026 12:20Waziri wa Urithi wa Utamaduni, Utalii na Kazi za Mikono wa Iran, Seyyed Reza Salehi-Amiri, amesema Afrika Kusini inaweza kuwa lango la Iran kuingia katika soko la utalii barani Afrika, akisisitiza umuhimu wa kubadilisha mazungumzo ya kisiasa na kidiplomasia kuwa ushirikiano wa kivitendo na wa kiuchumi.
-
Iran yaendelea kuboresha sekta yake ya ulinzi baada ya vita vya Marekani na Israel
Aug 22, 2026 02:55Wizara ya Ulinzi ya Iran imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu inaendelea kuifanya sekta yake ya ulinzi kuwa ya kisasa, ikizingatia mahitaji yaliyojitokeza kutokana na vita vya hivi karibuni vilivyolazimishwa dhidi ya nchi hii na Marekani na Israel.
-
Iran: Vikwazo vipya vya Marekani ni ‘ugaidi wa kiuchumi’ na ‘uhalifu dhidi ya ubinadamu’
Aug 21, 2026 10:34Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali mzunguko mpya wa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hili, ikisisitiza kuwa hatua hizo ni sawa na “ugaidi wa kiuchumi” na “uhalifu dhidi ya ubinadamu.”
-
Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran: Qur’ani yahimiza mshikamano wa Umma wa Kiislamu
Aug 21, 2026 10:29Imamu wa muda wa Swala ya Ijumaa mjini Tehran, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Muhammad-Hassan Abutorabi-Fard, amesema Wiki ya Umoja na sherehe za kukumbuka kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad (SAW) hutoa fursa muhimu ya kutafakari ujumbe wa Qur’ani Tukufu kuhusu umoja na mshikamano wa jamii ya Kiislamu.
-
Araghchi: “Ugaidi wa kiuchumi” wa Trump dhidi ya Iran ni mbinu ya kupotosha umma kuhusu matatizo ya uchumi wa Marekani
Aug 21, 2026 06:13Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ameionya Marekani kwamba kuendeleza sera “zilizoshindwa” dhidi ya Iran kutasababisha kurudi nyuma zaidi kwa Washington. Kauli hiyo imekuja huku Marekani ikigeukia mashinikizo ya kiuchumi baada ya kukiri kushindwa katika uchokozi wake wa kijeshi dhidi ya Iran.
-
Lengo la Marekani ni kupora rasilimali za eneo, Qalibaf amwambia Rais wa Iraq
Aug 21, 2026 06:10Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, amesema kuwa uwepo wa Marekani katika Ghuba ya Uajemi unasukumwa na shauku ya kupora rasilimali za eneo hilo.