Jeshi la Iran lalenga vituo vya jeshi la Marekani kujibu uchokozi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i139480-jeshi_la_iran_lalenga_vituo_vya_jeshi_la_marekani_kujibu_uchokozi
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limeendesha oparesheni kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya vituo nane vya kijeshi vya Marekani katika kanda hii, likiitaja hatua hiyo kuwa “jibu madhubuti” dhidi ya uchokozi mpya wa Marekani kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-06-28T04:35:41+00:00 )
Jun 28, 2026 04:34 UTC
  • Kombora la Iran likuvurumishwa kuekelea kambi ya jeshi la kigaidi la Marekani
    Kombora la Iran likuvurumishwa kuekelea kambi ya jeshi la kigaidi la Marekani

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa limeendesha oparesheni kubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani (droni) dhidi ya vituo nane vya kijeshi vya Marekani katika kanda hii, likiitaja hatua hiyo kuwa “jibu madhubuti” dhidi ya uchokozi mpya wa Marekani kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Katika taarifa yake, IRGC imebainisha kuwa oparesheni hiyo imetekelezwa na vikosi vyake “saa nane hadi tisa usiku wa Jumapili ,” na kulenga vituo nane “muhimu vya kijeshi vya Marekani,” vikiwemo “Kituo cha Anga cha Ali Al Salem nchini Kuwait” na “makao makuu ya Kamandi ya  Tano ya Wanamaji wa Marekani katika Bandari ya Salman nchini Bahrain.”

IRGC imethibitisha kuwa oparesheni hiyo ilihusisha makombora ya balistiki na droni, na kwamba vifaa vilivyolengwa vimeharibiwa kikamilifu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hatua hiyo imekuja kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na adui dhidi ya vituo vitano vya ulinzi vya pwani vya Iran mapema usiku kwa kuamikia leo.

Taarifa hiyo ilieleza: “Adui mchokozi, ambaye asili yake imejengeka katika kuvunja ahadi na kukiuka mikataba, ameshambulia vituo vitano vya pwani vya Jamhuri ya Kiislamu mapema leo, kwa kisingizio cha kujibu hatua ya Jeshi la Majini la IRGC ya kukabiliana na meli iliyokiuka mipaka katika Lango Bahari wa Hormuz].”

IRGC imesisitiza kuwa usafiri wa baharini kupitia Lango-Bahari la Hormuz uko chini ya dhamana ya Iran, kwa mujibu wa Mkataba wa Maelewano uliopatanishwa na Pakistan na kusainiwa hivi karibuni kati ya Iran na Marekani.

IRGCImeongeza kuwa, “Kuanzia sasa, meli zitakazokiuka sheria zitashughulikiwa kwa ukali zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.”

IRGC imesisitiza zaidi, “Adui anapaswa kufahamu kuwa kukiuka mapatano ya usitishaji vita ni kukiuka Ibara ya Kwanza ya Makubaliano ya Islamabad na kutaibua usitishaji kamili wa michakato yote inayohusiana na makubaliano hayo.”

Taarifa hii imetolewa kufuatia tangazo kutoka kwa Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM) kwamba ilifanya uchokozi mpya dhidi ya malengo yaliyomo ndani ya Iran.

CENTCOM ilidai kuwa mashambulizi hayo yalifanywa kama jibu kwa hatua ya kulengwa kwa meli ya kibiashara ya mafuta.

Muda mfupi baada ya tangazo hilo, shirika la utangazaji la Iran (IRIB), likinukuu duru za kijeshi zenye mamlaka, liliripoti milipuko katika Kaunti ya Sirik katika mkoa wa kusini wa Hormozgan.

Wakazi pia waliripoti kusikia milipuko kadhaa katika Kisiwa cha Qeshm, ingawa maeneo kamili na sababu za milipuko hiyo hazikujulikana mara moja, kulingana na ripoti hiyo.

Mvutano huu mpya unafuatia tukio la Ijumaa ambapo Jeshi la Majini la IRGC lilifyatua risasi za onyo kwa meli iliyopuuza maonyo dhidi ya kutumia njia isiyoidhinishwa katika Lango Bahari

Vikosi vya Marekani vimekuwa vikikiuka mara kwa mara usitishaji vita uliotangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump mnamo Aprili 7.