-
IRGC: Vikizuka vita vipya, Iran itatumia silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa zaidi
Aug 20, 2026 11:51Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetangaza kuwa, kama vitazuka vita vipya litatumia silaha zinazosababisha uharibifu mkubwa zaidi na za kisasa zaidi kuliko zile zilizotumika katika vita vilivyopita.
-
Ripoti: Vita vikishtadi, yamkini Iran ikavishambulia vituo vya Marekani barani Ulaya
Aug 20, 2026 11:46Gazeti la Financial Times limeripoti kuwa Iran inafikiria kushambulia vituo vya kijeshi vya Marekani barani Ulaya ikiwa Rais wa Marekani Donald Trump atashadidisha vita, wakati Tehran inazingatia pia machaguo ya kupanua wigo wa mzozo hadi nje ya Mashariki ya Kati.
-
Namna shambulio la kijeshi dhidi ya Iran lilivyoikatisha tamaa Ulaya
Aug 20, 2026 06:39Vita vinavyoendeshwa na Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran si mgogoro wa kijeshi wa eneo dogo tu katika Asia Magharibi. Kufungwa Lango-Bahari la Hormuz na kuvurugika kimataifa usambazaji wa nishati kumetikisa uchumi wa dunia nzima, ambapo madhara yake yanaonekana wazi hadi katika kitovu cha Ulaya na Uingereza.
-
Spika Qalibaf: Muqawama wa Iraq ni chanzo kikuu cha nguvu kwa Iran na Iraq
Aug 20, 2026 03:30Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf amesema Muqawama wa Kiislamu nchini Iraq umekuwa moja ya nguzo muhimu za nguvu kwa Iran na Iraq, akisisitiza kuwa fikra na harakati za Muqawama zimevuka mipaka ya eneo na kupata uungwaji mkono duniani.
-
Kamanda wa majeshi ya Iran azionya nchi za Ghuba ya Uajemi kuhusu kulisaidia jeshi la Marekani
Aug 19, 2026 11:03Mkuu wa Majeshi ya Iran amezionya nchi za kusini mwa Ghuba ya Uajemi kuhusu kulisaidia au kuliruhusu jeshi la Marekani kutumia ardhi za nchi hizo katika uchokozi wake dhidi ya Iran.
-
Iran yawatimua wanadiplomasia wawili wa Ufaransa kutokana na mienendo yao haramu
Aug 19, 2026 10:05Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imewatangaza wanadiplomasia wawili wa Ufaransa wanaofanya kazi katika Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran kuwa ni watu wasiostahili kutokana na shughuli zao zinazotambuliwa kuwa kinyume na sheria za kimataifa na Mkataba wa Vienna wa 1961 kuhusu Mahusiano ya Kidiplomasia.
-
Iran yamtahadharisha Trump kuhusu 'fikra potofu' ya kudai Mlango-Bahari wa Hormuz ni eneo la Marekani
Aug 19, 2026 04:16Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia Masuala ya Kisheria na Kimataifa Kazem Gharibabadi amemkosoa vikali Rais Donald Trump wa Marekani kwa madai yake kuhusu Lango la Bahari la Hormuz, akionya kuwa "fikra yake potofu" ya kuihesabu njia hiyo muhimu ya maji kama "eneo jipya la Marekani" inapasa kurekebishwa, la sivyo Tehran itamweka sawa.
-
Marasimu ya Arubaini ya kumuenzi Kiongozi shahidi wa Iran na familia yake yafanyika Musalla wa Imam Khomeini, Tehran
Aug 18, 2026 15:39Sambamba na kutimia siku arubaini tangu kufanyika mazishi ya kihistoria ya kiongozi wa Iran aliyeuliwa shahidi, shughuli ya kumbukumbu ya kumuenzi kiongozi huyo shahidi na familia yake imefanyika leo katika eneo la Swala (Mosalla) la Imam Khomeini (RA) mjini Tehran.
-
Pezeshkian: Ustahimilivu, umoja, na matumaini ni nguzo ya Iran kukabiliana na vitisho vya nje
Aug 18, 2026 11:43Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema vita vya Iraq dhidi ya Iran, vinavyofahamika nchini Iran kama Vita vya Kujihami Kutakatifu, vina somo muhimu ambalo ni ustahimilivu, umoja, na matumaini.
-
Qalibaf: Iran italipiza kisasi damu ya Kiongozi Shahidi
Aug 18, 2026 11:41Spika wa Bunge la Iran, Mohammad Baqer Qalibaf, ameahidi kwamba Jamhuri ya Kiislamu haitaruhusu damu ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliyeuawa shahidi, Ayatollah Sayyid Ali Khamenei, na mashahidi wengine wa uvamizi wa Marekani na Israel dhidi ya taifa hili “kupotea bila kulipiziwa kisasi.”