-
Timu ya taifa ya karate ya wanawake ya Iran yatwaa ubingwa wa Asia
Jun 22, 2026 04:33Timu ya taifa ya karate ya wanawake ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetwaa ubingwa wa bara la Asia katika mchezo huo.
-
Iran yasema mazungumzo na Marekani yanahusu kutotekelezwa kwa kifungu cha kwanza cha makubaliano
Jun 21, 2026 11:26Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesema kuwa mazungumzo yaliyopangwa kufanyika na Marekani yatalenga suala la kutotekelezwa kwa kifungu cha kwanza cha Waraka wa Makubaliano (MoU) uliosainiwa hivi karibuni kati ya nchi hizo mbili.
-
Mshauri wa Kiongozi aonya dhidi ya matumaini kupita kiasi kuhusu mazungumzo na “adui anayevunja ahadi”
Jun 21, 2026 11:24Mshauri mwandamizi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonya dhidi ya kuwa na matumaini kupita kiasi kuhusu mazungumzo na adui, akitaja historia yake ya kuvunja ahadi.
-
Spika wa Bunge la Iran aapa kuwa mwaminifu kwa mashahidi baada ya kuwasili Uswisi kwa mazungumzo na US
Jun 21, 2026 04:41Spika wa Bunge la Iran amesisitiza tena kwamba atatetea haki za Wairani waliouawa shahidi wakati wa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu baada ya kuwasili Uswisi kufuatilia mkataba wa Hati ya Maelewano uliosainiwa na viongozi wa nchi mbili kwa lengo la kukomesha vita.
-
Picha ya mazishi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Minab yashinda tuzo ya picha bora zaidi ya mwaka
Jun 21, 2026 02:58Picha iliyochukuliwa kutokea angani inayoonyesha mazishi ya wanafunzi 168 waliouawa shahidi wakati wa shambulio la makombora ya Marekani dhidi ya Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab, kusini mwa Iran, imeshinda tuzo ya juu katika Kategoria ya Upigaji Picha za Habari ya tuzo za Golden Shot Photography Awards 2026.
-
Iran yafunga tena Lango-Bahari la Hormuz baada ya Marekani na Israel kukiuka MoU
Jun 20, 2026 14:46Kamandi Kuu ya Majeshi ya Iran imetangaza rasmi kwamba Lango-Bahari la Hormuz limefungwa kwa vyombo vyote vya usafirishaji wa baharini, baada ya Marekani na Israel kukiuka makubaliano ya hati ya maelewano ya kusitisha vita kati ya Tehran na Washington.
-
Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Iran ya kushukuru ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kuhusu mazungumzo ya Iran na Marekani
Jun 20, 2026 13:00Katika kujibu ujumbe wa Kiongozi muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu mazungumzo ya Iran na Marekani, Wizara ya Ulinzi na Msaada Kwa Jeshi la Iran imesisitiza katika taarifa kwamba: Siri ya mafanikio endelevu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kufuata kamilifu na bila kusitasita amri na hatua za Amiri Jeshi Mkuu.
-
Waziri wa mambo ya ndani wa Pakistan arejea tena Tehran kujadili mazungumzo ya Iran na Marekani
Jun 20, 2026 12:10Syed Mohsin Raza Naqvi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan amerejea tena Tehran kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na viongozi wa ngazi za juu wa Iran, kuhusu suala la kuendeleza mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani.
-
Bunge la Iran: Ukiukaji wowote wa ahadi wa Marekani utakabiliwa na jibu kali
Jun 20, 2026 12:08Mwenyekiti wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran ameandika katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii kwamba: "Ukiukaji wowote wa ahadi utakaofanywa na Marekani au kujiondoa katika fremu kuu ya maelewano kutapelekea jeshi la Iran, kwa uungaji mkono wa taifa shupavu la Iran kutoa jibu kali, thabiti na la kuumiza zaidi dhidi ya adui huyo kuliko ilivyokuwa huko nyuma."
-
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Amani na uthabiti nchini Lebanon na eneo havitapatikana bila ya kukomeshwa uvamizi wa adui
Jun 20, 2026 12:05Katika mahojiano na televisheni ya Al Jazeera, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa: Washington lazima imzuie Netanyahu kuvuruga juhudi za maelewano kwa sababu hakuna amani wala utulivu wowote utakaopatikana Lebanon na katika eneo zima la Asia Magharibi bila kukomeshwa uvamizi na ukaliaji mabavu wa ardhi za nchi za eneo.