-
Raisi: Siku ya Kimataifa ya Quds ni nembo ya kuwatimua Wazayuni katika ardhi za Palestina
Apr 04, 2024 04:22Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameitaja Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa ni ukumbusho wa kukaribia ushindi wa mwisho wa wananchi wa Palestina dhidi ya wavamizi wa Kizayuni na ishara ya mshikamano, umoja na uelewa wa Umma wa Kiislamu katika kutatua kadhia ya Palestina na kuwafukuza wavamizi kutoka katika ardhi zote za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran akosoa upuuzaji wa Umoja wa Ulaya kuhusu ugaidi wa Israel
Apr 04, 2024 04:18Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa misimamo ya undumakuwili ya Umoja wa Ulaya na upuuzaji wake kuhusiana na jinai na vitendo vya kigaidi vya utawala ghasibu wa Israel.
-
Shambulio la kigaidi kusini mashariki mwa Iran
Apr 04, 2024 04:03Alireza Marhamati, Naibu Gavana anayesimamia masuala ya usalama na utekelezaji sheria katika mkoa wa Sistan na Baluchistan, kusini mashariki mwa Iran, ametangaza kutokea shambulio la kigaidi kwenye makao makuu mawili ya kijeshi katika miji ya Rask na Chabahar mkoni humo.
-
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Israel itazabwa kibao usoni kwa shambulio lake dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria
Apr 03, 2024 23:48Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema utawala wa Kizayuni wa Israel utazabwa kibao usoni kutokana na shambulio lake dhidi ya majengo ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria, mapema wiki hii.
-
Mazishi ya washauri wa kijeshi wa Iran waliouawa katika hujuma ya Israel jijini Damascus
Apr 03, 2024 08:48Maelfu ya watu wameshiriki katika msafara wa mazishi ya washauri wa kijeshi wa Iran, waliouawa shahidi katika shambulizi la makombora la utawala haramu wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran katika mji mkuu wa Syria Damascus.
-
Baraza la Usalama UN lalaani mashambulizi ya Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran, Damascus
Apr 03, 2024 07:19Wawakilishi waliohudhuria kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran huko Damascus (mji mkuu wa Syria) wamelaani kitendo hicho cha kinyama cha Wazayuni.
-
Rais Ebrahim Raisi: Israel iko kwenye sakaratul mauti, inakata roho
Apr 03, 2024 03:39Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, shambulio la juzi Jumatatu la utawala wa Kizayuni kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus Syria ni ushahidi kuwa Israel iko kwenye sakaratul mauti na inakata roho hivi sasa.
-
Katibu Mkuu wa UN alaani shambulio la Israel lililolenga ubalozi mdogo wa Iran Damascus
Apr 02, 2024 23:15Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amelaani shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya sehemu ya ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus, Syria na kuonya kwamba mahesabu yoyote ya kimakosa yanaweza kusababisha mapigano yenye wigo mpana zaidi katika eneo hili tete na lisilo na uthabiti na kusababisha matokeo haribifu kwa raia.
-
Kiongozi Muadhamu: Iran itaufanya utawala wa Israel ujutie uhalifu nchini Syria
Apr 02, 2024 10:01Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Majenerali walioongoka wa Kiislamu katika shambulio la utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ubalozi mdogo wa Iran nchini Syria na kusisitiza kwamba: "Taifa la Iran litawafanya Wazayuni wajutie jinai hiyo na jinai zingine kama hiyo."
-
Matokeo ya kieneo na kimataifa ya shambulio la kigaidi la utawala wa Kizayuni kwenye ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus.
Apr 02, 2024 08:14Shambulio la kigaidi la ndege za kivita za utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Damascus bila shaka litakuwa na matokeo ya kieneo na kimataifa kwa baraza la mawaziri la kuchochea vita la Benjamin Netanyahu.