-
Ebrahim Raisi: Kuchochea machafuko na ugaidi nchini Iran si kwa manufaa ya Marekani wala Magharibi
Nov 20, 2022 23:23Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuchochea machafuko na ugaidi nchini Iran si kwa manufaa ya Wamarekani wala nchi za Magharibi na ametoa amri kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuyafuatilia kidiplomasia na kisheria madola yote yaliyohusika na machafuko na vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni nchini Iran.
-
Kan'ani: Malengo ya vita vya vyombo vya habari ni kuwasafisha wahalifu washirika wa Marekani
Nov 20, 2022 06:56Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa malengo ya vita vya vyombo vya habari na mashinikizo ya kisiasa ya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwatakasa wahalifu wenye mfungamano na Marekani.
-
Maelfu Mashhad nchini Iran wahudhuria mazishi ya mashahidi watatu waliouawa katika ghasia
Nov 20, 2022 04:29Wakazi wa mji wa kaskazini mashariki mwa Iran wa Mashhad wamehudhuria msafara wa mazishi ya wanachama wawili wa kikosi cha kujitolea cha wananchi cha Basij na mwanajeshi mmoja, ambao waliuawa na waasi siku chache zilizopita.
-
Rais wa Iran asema Marekani inashindwa kutokana na maendeleo ya Wairani lakini bado haijifunzi kutokana na hilo
Nov 20, 2022 01:54Rais Ebrahim Raisi wa Iran amesema Marekani imeshindwa mbele ya maendeleo makubwa yaliyofanywa na taifa la Iran katika kipindi cha miongo minne iliyopita lakini bado haijajifunza kutokana na kushindwa kwake huko.
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Shari bila shaka itasambaratishwa
Nov 19, 2022 08:56Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema lengo kuu la wachochezi wa machafuko ya hivi karibuni ni kuliingiza taifa la Iran katika medani na kuongeza kuwa: "Mchafuko hayo bila shaka yatakomeshwa na taifa kuendelea kusonga mbele kwa nguvu zaidi na ari mpya katika uwanja wa maendeleo ya nchi."
-
Russia na China zapinga azimio la Bodi ya Magavana ya Wakala wa IAEA dhidi ya Iran
Nov 19, 2022 08:22Azimio jipya la Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran yenye malengo ya amani limepasishwa ambapo limetuma ujumbe ulio wazi kufuatia kupungua kwa kura za nchi zilizoliunga mkono licha ya mashinikizo mapya ya kisiasa ya Marekani na Troika ya Ulaya dhidi ya Iran.
-
Haki za taifa la Iran zimekiukwa kwa vikwazo vya Marekani dhidi ya IRIB, Press TV
Nov 19, 2022 08:00Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan’ani, amelaani uamuzi wa hivi karibuni wa Marekani wa vikwazo vinavyolenga Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (IRIB) na Televisheni ya Press TV akisema ni ukiukaji wa haki za taifa la Iran.
-
Kunyamazia mashambulio ya kigaidi yanayofanywa Iran hakuna tija nyingine isipokuwa kuimarisha ugaidi
Nov 19, 2022 04:17Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa ambayo mbali na kulaani vitendo vya kigaidi katika miji ya Izeh, Esfahan na Mashhad imesisitiza kuwa: hakuna shaka kuwa kimya cha makusudi cha waenezaji fujo na machafuko ndani ya Iran wa kutokea nje ya nchi mbele ya hujuma zillizo dhahir shahir za kigaidi zilizofanywa katika miji kadhaa ya Iran, hakina matokeo mengine isipokuwa kuimarisha ugaidi ulimwenguni.
-
Kapteni wa timu ya Iran: Vyombo vya habari vya Uingereza vimeanzisha vita vya kisaikolojia
Nov 19, 2022 03:42Nahodha wa timu ya taifa ya kandanda ya Iran katika Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar amesema, vyombo vya habari vya Uingereza vimeanzisha mchezo wa vita vya kisaikolojia sambamba na kukaribia mechi kati ya timu ya nchi hiyo na Iran.
-
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Iran: Hatua za kinyama za kuwaua walinda amani hazitaachwa bila kujibiwa
Nov 19, 2022 00:30Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu mauaji ya kinyama ya walinzi wawili wa amani katika mji wa Mashhad makao makuu ya mkoa wa Khorasani-Razavi, kaskazini mashariki ya nchi, kwamba hatua kama hizo zisizo za kiutu hazitaachwa bila kujibiwa.