-
Majasusi wawili wa Ufaransa wakiri majaribio ya kuchochea ghasia nchini Iran
Oct 07, 2022 04:24Majasusi wawili wa Ufaransa waliokamatwa nchini Iran takriban miezi minne iliyopita wamekiri majaribio yao ya kuzusha maandamano na ghasia dhidi ya serikali kwa lengo kuu la kuweka shinikizo dhidi ya mfumo wa Kiislamu nchini.
-
Brigedia Jenerali Ashtari: Usalama wa wananchi ni mstari wetu mwekundu
Oct 06, 2022 23:05Kamanda wa Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa mtu au kundi lolote linalotaka kuvuruga na kuvuruga usalama wa watu, litakabiliwa na walinzi wa amani na usalama wa wananchi, na walinzi hao wa amani watakuwa pamoja bega kwa bega na wananchi.
-
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran: Dunia haijasahau kashfa ya makaburi ya halaiki nchini Canada
Oct 06, 2022 10:15Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema: Ulimwengu bado haujasahau kashfa ya kugunduliwa kwa makaburi ya halaiki ya mamia ya watoto katika viwanja vya shule za wamishonari yapata mwaka mmoja uliopita.
-
Kamanda wa IRGC: Maadui wameungana kuvuruga usalama wa Iran ya Kiislamu
Oct 06, 2022 06:22Naibu kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameashiria ghasia za hivi karibuni katika baadhi ya miji ya Iran na kusema kuwa katika fitna hiyo maadui wote waliingia uwanjani ili kuifanya Iran ya Kiislamu kutokuwa salama.
-
Abdollahian: Serikali itakabiliana na wafanya fujo, magaidi kwa misingi ya sheria
Oct 06, 2022 04:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameuonya Umoja wa Ulaya dhidi ya kuingilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu na kusisitiza kuwa, serikali ya Tehran itakabiliana na wafanya fujo na magaidi kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi hii.
-
Iran: Tutatoa jibu iwapo EU itaendelea na tabia yake ya uingiliajii
Oct 06, 2022 00:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametahadharisha kuwa, Tehran itatoa jibu mwafaka iwapo Umoja wa Ulaya utaendelea na tabia yake ya kungilia masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran yamwita tena balozi wa Uingereza kulalamikia matamshi ya uingiliaji ya London
Oct 05, 2022 09:28Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imemwita balozi wa Uingereza mjini Tehran, Simon Shercliff, kwa mara ya pili katika muda wa chini ya wiki mbili kutokana na uingiliaji wa London katika masuala ya ndani ya Iran.
-
Nasser Kan'ani: Morocco iwajibike kwa madhara ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu
Oct 05, 2022 03:38Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amemwambia Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Morocco kwamba anapaswa kuwajibishwa kutokana na ukosefu wa usalama unaotokana na kuanzisha uhusiano baina ya nchi hiyo na na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kuua watu wa Palestina na kukalia kwa mabavu kibla cha kwanza cha Waislamu.
-
Iran yamtaka Biden ashughulikie rekodi chafu ya haki za binadamu Marekani
Oct 04, 2022 22:47Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekosoa vikali unafiki wa Marekani katika masuala ya haki za binadamu. Aidha amemtaka Rais Joe Biden wa Marekani ashughulikie rekodi mbaya ya haki za binadamu ya nchi yake na aondoe vikwazo vilivyo dhidi ya ubinadamu ilivyoiwekea Iran iwapo kweli anajali haki za binadamu.
-
Iran yafanyia jaribio chombo kipya cha kubeba satalaiti
Oct 04, 2022 22:41Iran imefanyia majaribio chombo kilichobuniwa na kutengenezwa nchini chenye uwezo wa kuhamisha satalaiti zilizo katika anga za mbali kutoka sehemu moja hadi nyingine.