-
Rais Rouhani: Taifa la Iran litalipiza kisasi cha kuuliwa kigaidi, shahid Fakhrizadeh
Nov 28, 2020 08:17Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, maadui wote watambue kwamba, wananchi na viongozi wa Iran ni mashujaa na wenye ghera kubwa, hivyo lazima watalipiza kisasi cha vitendo vya jinai linavyofanyiwa taifa hili la Kiislamu.
-
Mauaji ya kigaidi ya Mohsen Fakhrizadeh; kukaririwa senario iliyofeli ya kuzuia ustawi wa kielimu nchini Iran
Nov 28, 2020 07:34Mohsen Fakhrizadeh ambaye alikuwa Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliuawa Ijumaa alasiri katika moja ya viunga vya mji mkuu, Tehran.
-
Kiongozi Muadhamu: Watieni adabu waliofanya na kuamrisha jinai ya kuuliwa kigaidi shahid Fakhrizadeh
Nov 28, 2020 06:12Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametilia mkazo wajibu wa kutiwa adabu na kupewa adhabu isiyoepukika wote waliofanya na kuamrisha mauaji ya kigaidi ya mwanasayansi wa Kiirani, Dk. Mohsen Fakhrizadeh.
-
Rais Rouhani: Mauaji ya wanasayansi wa nyuklia yanatokana na maadui kushindwa mtawalia
Nov 28, 2020 04:37Rais Hassan Rouhani amesema, hapana shaka tukio la kigaidi na la kutapatapa la mauaji ya wanasayansi wa nyuklia linatokana na kushindwa na kuemewa maadui waliolikamia taifa la Iran.
-
Iran italipiza kisasi mauaji ya mwanasayansi maarufu, shahidi Fakhrizadeh
Nov 28, 2020 01:21Waziri wa Intelijensia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa Iran italipiza kisasi kufuatia kuuawa shahidi Mohsen Fakhrizadeh ambaye alikuwa Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu katika Wizara ya Ulinzi ya Iran.
-
Iran yafafanua mchakato wa kuachiwa huru raia wake 3 kwa kubadilishana na jasusi wa Israel
Nov 27, 2020 09:02Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na masuala ya kisiasa ametoa ufafanuzi kuhusu namna raia watatu wa Iran walivyoachiwa huru mkabala na Jamhuri ya Kiislamu kumwachia jasusi wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Rais Rouhani: Iran inaweza kuyadhaminia mataifa ya dunia mahitaji yao kwa bei rahisi zaidi
Nov 26, 2020 08:14Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Tehraninao uwezo wa kulidhaminia eneo hili na hata dunia nishati ya bei rahisi zaidi
-
Ghanei: Iran ina uwezo wa utafiti wa kisayansi na kitiba wa kiwango cha juu katika eneo
Nov 26, 2020 04:25Mkuu wa Kamati ya Kielimu ya Idara ya Kitaifa ya Kupambana na Virusi vya Corona nchini Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kiutafiti wa kiwango cha juu katika uwanja wa sayansi na tiba khususan baina ya nchi za eneo.
-
Rouhani: Nia ya Iran ni kuwa na uhusiano wa kiudugu na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi
Nov 26, 2020 00:24Rais Hassan Rouhani amesema uhusiano wa Iran na Qatar ni wa kirafiki na unaendelea kustawi na akasisitiza kwamba inachotaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa na mazungumzo, maelewano na uhusiano wa kiudugu na nchi za pembezoni mwa Ghuba ya Uajemi.
-
Rais Rouhani: Serikali ijayo ya Marekani ifidie makosa yaliyotangulia
Nov 25, 2020 08:49Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria ushindi wa wananchi wa Iran na kushindwa adui katika vita vyake vya kiuchumi dhidi ya taifa hili na kueleza kwamba, serikali ijayo ya Marekani inapaswa kulaani waziwazi sera na hatua zisizo za kibinadamu na kigaidi za Donald Trump na ifidie siasa hizo zisizo sahihi.