-
Sisitizo la Kiongozi wa Mapinduzi la "kuzima makali ya vikwazo na kuvishinda" badala ya kutumainia madola ya kigeni
Nov 25, 2020 07:23Jana Jumanne tarehe 24 Novemba Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alikutana na kuzungumza na viongozi wa mihimili mikuu mitatu ya dola pamoja na wajumbe wengine wa Baraza Kuu la Uratibu wa Uchumi, ambapo katika hotuba yake kwa viongozi hao alibainisha nukta kadhaa muhimu na za kimkakati kuhusu masuala ya kiuchumi ya nchi.
-
Kiongozi Muadhamu: Basij ni utajiri mkubwa na hazina liliyotunukiwa na Mungu taifa la Iran
Nov 25, 2020 04:11Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, jeshi la kujitolea la Basij ni utajiri mkubwa na hazina liliyotunukiwa na Mwenyezi Mungu taifa la Iran.
-
Chanjo za corona za Iran zasajiliwa katika Shirika la Afya Duniani
Nov 24, 2020 23:47Katibu wa kamati ya sayansi ya tume ya taifa ya kukabiliana na corona nchini Iran amesema, chanjo za ugonjwa wa Covid-19 zilizotengenezwa hapa nchini zimesajiliwa katika Shirika la Afya Duniani (WHO).
-
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Huwezi kuyaamini kikamilifu madola ya kigeni
Nov 24, 2020 09:40Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Haiwezekani kuwa na imani kamili na madola ya kigeni na kuwa na matumaini nayo kwa ajili ya kutatua matatizo.
-
Wimbi la maambukizo ya corona limeanza kupungua nchini Iran
Nov 24, 2020 03:54Mjumbe mmoja wa Kamati ya Taifa ya Kupambana na Corona nchini Iran amesema kuwa, takwimu za karibuni kabisa zinaonesha kuwa wagonjwa wa COVID-19 wanaoripoti katika vituo vya matibabu humu nchini wamepungua kwa asilimia 30 hadi 40 ikilinganishwa na wiki iliyopita.
-
Mousavi: Iran ina hamu ya kuona utulivu na amani inatawala katika eneo hili zima
Nov 24, 2020 03:48Msemaji wa zamani wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye sasa ni balozi wa Iran nchini Azerbaijan amesema kuwa, Tehran ina hamu ya kuona utulivu na amani ya kudumu inapatikana katika eneo hili zima.
-
Ghalibaf: Vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi huru, ni siasa zilizofeli
Nov 23, 2020 22:54Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, vikwazo vya Marekani dhidi ya nchi huru duniani ni siasa zilizofeli na kuongeza kuwa, vikwazo hivyo vimeimarisha misingi ya uchumi wa kutengemea uwezo wa ndani, nchini Iran.
-
Raisi: Haki za binadamu zinatumiwa kama wenzo wa kuzishinikiza nchi huru duniani
Nov 23, 2020 09:46Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Iran amesema kuwa Canada inakiuka haki za binadamu na ni kimbilio la mafisadi na wahalifu. Ameongeza kuwa nchi mbaimbali duniani zimetambua kwamba haki za binadamu zimetiwa siasa kali na kugeuzwa wenzo wa kuziweka chini ya mashinikizo nchi huru duniani.
-
Khatibzadeh: Yeyote atakayekuweko White House hatakuwa na chaguo isipokuwa kuheshimu haki za taifa la Iran
Nov 22, 2020 09:05Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa, yeyote atakyekuweko Ikulu ya White House hatakuwa na chaguo jengine isipokuwa kuheshimu haki za taifa la Iran.
-
Majibu ya Iran kwa upayukaji na tuhuma za nchi za Ulaya zilizomo kwenye JCPOA
Nov 22, 2020 06:09Baada ya Marekani kujitoa katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA hapo tarehe 8 Mei 2018 na kuirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyoondolewa baada ya mapatano hayo, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilisubiri mwaka mzima kuona wanachama waliobakia ndani ya JCPOA hasa nchi tatu za Ulaya, watachukua hatua gani za kukabiliana na ubeberu huo wa Marekani, lakini hakuna walichofanya.