-
Iran: Shambulio la kigaidi la Kabul ni mfano wa vita vya niaba vya Marekani nchini Afghanistan
Nov 22, 2020 00:43Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, shambulio la kigaidi la Kabul ni mfano mmojawapo wa vita vya niaba na hatua zinazochukuliwa na waitifaki wa utawala wa kigaidi wa Marekani nchini Afghanistan.
-
Watu wengine 431 wameaga dunia kwa corona nchini Iran
Nov 21, 2020 08:42Msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema kuwa, watu wengine zaidi ya elfu 12 wameambukizwa virusi vya corona na wengine 431 wamefariki dunia katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
-
Kuongezeka nguvu ya kiulinzi ya Iran katika kivuli cha mashinikizo ya juu kabisa ya Marekani
Nov 21, 2020 07:06Siasa imara na za busara za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mkabala na Marekani zimepelekea siasa laini na ngumu za Washington kukabiliwa na changamoto kubwa.
-
Iran yakanusha madai ya kuzungumza na timu ya Joe Biden
Nov 20, 2020 23:57Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekadhibisha ripoti iliyochapishwa na gazeti la New York Times la Marekani kwamba Tehran imewasiliana na timu ya Rais mteule wa nchi hiyo, Joe Biden.
-
Iran: Utawala wa Kizayuni ujiunge haraka na mkataba wa nyuklia wa NPT
Nov 20, 2020 09:08Mjumbe na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yao mjini Vienna, Austria ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ujiunge haraka na Mkataba za Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia NPT, tena bila ya masharti yoyote.
-
Meja Jenerali Salami: Ghuba ya Uajemi ni ngome imara ya kujilinda Iran ya Kiislamu
Nov 19, 2020 07:45Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema kuwa Ghuba ya Uajemi ni ukanda wenye nguvu wa kuilinda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na ni makutano ya makabilianao baina ya madola.
-
Zarif: Iran iko tayari kuzungumzia masharti ya kuirejesha Marekani kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA
Nov 18, 2020 23:48Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran iko tayari kufanya mazungumzo ya kujadili masharti na namna ya kuirejesha Marekani kwenye mazungumzo ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji, JCOPA.
-
Rouhani: Utawala wa sasa wa Marekani ni wa kijinai na kigaidi
Nov 18, 2020 08:31Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuhusu mienendo haribifu na ugaidi wa kiuchumi wa Washington na kusema kuwa, utawala ulioko madarakani hivi sasa nchini Marekani ni mtenda jinai na dola la kigaidi.
-
Gharibabadi amhutubu Adel al Jubair: Usiwalaumu wengine kwa hatua zako ghalati
Nov 18, 2020 04:24Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika taasisi za kimataifa zenye makao yake mjini Vienna Austria jana usiku alijibu matamshi ya karibuni dhidi ya Iran ya Adel al Jubair Waziri Mshauri Katika Masuala ya Nje wa Saudi Arabia kwa kusema: Iwapo Riyadh inataka kuwa na miradi ya nyuklia au kuibua kisingizio kwa ajili ya kuhalalisha kutoshirikiana na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) basi iwe na uthubutu wa kulipa gharama zake.
-
Iran yaonya kutoa jibu kali kwa chokochoko zozote za Marekani
Nov 18, 2020 04:07Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonya kutoa jibu kali kwa chokochoko na hatua yoyote ya kiuadui itakayochukuliwa na serikali ya Marekani dhidi ya maslahi yake ya kitaifa.