Rouhani: Utawala wa sasa wa Marekani ni wa kijinai na kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i64701-rouhani_utawala_wa_sasa_wa_marekani_ni_wa_kijinai_na_kigaidi
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuhusu mienendo haribifu na ugaidi wa kiuchumi wa Washington na kusema kuwa, utawala ulioko madarakani hivi sasa nchini Marekani ni mtenda jinai na dola la kigaidi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 18, 2020 12:01 UTC
  • Rouhani: Utawala wa sasa wa Marekani ni wa kijinai na kigaidi

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kuhusu mienendo haribifu na ugaidi wa kiuchumi wa Washington na kusema kuwa, utawala ulioko madarakani hivi sasa nchini Marekani ni mtenda jinai na dola la kigaidi.

Rais Rouhani amesema hayo leo Jumatano katika kikao cha Baraza la Mawaziri na kufafanua kuwa: Tangu serikali ya sasa ya Marekani ianzishe vita vya kiuchumi dhidi ya Iran, Tehran imekuwa chini ya mzingiro wa kiuchumi na kuandamwa na ugaidi wa kiuchumi wa Washington.

Amesema taifa hili limekuwa likikabiliana na utawala wa kibeberu katika miaka ya hivi karibuni, na kwamba licha ya Marekani kufanikiwa kuliweka taifa la Iran chini ya mashinikizo katika sekta ya uchumi, lakini imeshindwa kufikia lengo lake kuu la kuvuruga usalama wa ndani ya nchi hii.

Licha ya janga la corona ambalo limeitikisa dunia nzima, lakini utawala wa Rais Donald Trump umeshadidisha vikwazo na mashinikizo ya kiwango cha juu zaidi dhidi ya wananchi wa Iran katika kipindi hiki.

Maandamano ya kupinga vikwazo vya US dhidi ya Iran katika kipindi hiki cha janga la corona

Dakta Rouhani amesisitiza kuwa, hali ya kiuchumi na kijamii ya nchi hii inaendelea kuboreka siku baada ya siku, na serikali itaendelea kuchukua hatua za kuwapunguzia wananchi matatizo wanayokabiliana nayo.

Rais wa nchi hii ameashiria kuhusu hatua mpya za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona zitakazoanza kutekelezwa hapa nchini Jumamosi ijayo na kubainisha kuwa, serikali itatoa kifurushi cha msaada kwa thuluthi moja ya jamii ya Wairani watakaoathiriwa zaidi na hatua hizo, kwa muda wa miezi minne.