Mali yakanusha hofu kwamba magaidi wanakaribia kuudhibiti mji mkuu, Bamako
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i133126-mali_yakanusha_hofu_kwamba_magaidi_wanakaribia_kuudhibiti_mji_mkuu_bamako
Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali amepuuzilia mbali dhana kwamba magaidi hivi karibuni wanaweza kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako. Hii ni radiamali ya kwanza kutolewa na serikali kuhusu wasiwasi na hofu ya usalama katika nchi ya Mali ambayo imechochea nchi za Magharibi kuwataka raia wao waondoke nchini humo.
(last modified 2025-11-13T16:40:03+00:00 )
Nov 13, 2025 12:34 UTC
  •  Abdoulaye Diop
    Abdoulaye Diop

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali amepuuzilia mbali dhana kwamba magaidi hivi karibuni wanaweza kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako. Hii ni radiamali ya kwanza kutolewa na serikali kuhusu wasiwasi na hofu ya usalama katika nchi ya Mali ambayo imechochea nchi za Magharibi kuwataka raia wao waondoke nchini humo.

Nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika inapambana dhidi ya magaidi wa kundi la JNIM wenye mfungamano na mtandao wa al Qaida ambao mwezi Septemba walitangaza kile walichokitaja "uzuiaji wa mafuta" uliosababisha foleni ndefu katika vituo vya kuuzia petroli katika mji mkuu, Bamako. 

Uhaba huo wa mafuta ulipelekea kufungwa kwa muda shule katika mji mkuu huo wa Mali. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali, Abdoulaye Diop, amesema kuwa nchi hiyo imefanikiwa kupunguza athari za hujuma hiyo ya magaidi ya kuzuia uuzaji mafuta ya petroli mjini Bamako. 

Tarehe 9 mwezi huu Umoja wa Afrika ulitoa wito wa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo kukabiliana na hali mbaya ya ukosefu wa usalama katika mji mkuu wa Mali, Bamako. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali ameongeza kuwa wito wa Umoja wa Afrika kwamba kuna haja ya kuchukuliwa hatua katika ngazi ya kimataifa za kukabiliana na hali ya mambo ya Mali  ikiwa ni pamoja na kubadilishana taarifa za kiitelijinsia unaakisi ufahamu dhaifu wa kile kinaechondelea sasa nchini Mali.

Shule nyingi zilifunguliwa tena Jumatatu wiki hii, huku Bamako ikijiandaa kwa ajili ya maonyesha ya sekta ya ulinzi yanayozishirikisha kampuni kadhaa za masuala ya ulinzi za Uturuki. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali amesema kuwa anaheshimu wito wa baadhi ya nchi zilizowataka raia wao kuondoka Mali lakini akasisitiza kuwa Mali inaendelea kuwakaribisha wageni kutoka nje.