Polisi Kenya yathibitisha vifo vya watu 18 katika maporomoko ya ardhi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i138158-polisi_kenya_yathibitisha_vifo_vya_watu_18_katika_maporomoko_ya_ardhi
Huduma ya Polisi ya Kenya Jumapili ilithibitisha kupoteza maisha watu 18 kufuatia maporomoko ya udongo na mafuriko huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, na kulazimisha familia nyingi kuhama makazi yao.
(last modified 2026-05-04T10:25:30+00:00 )
May 04, 2026 10:21 UTC
  • Athari za mafuriko Kenya
    Athari za mafuriko Kenya

Huduma ya Polisi ya Kenya Jumapili ilithibitisha kupoteza maisha watu 18 kufuatia maporomoko ya udongo na mafuriko huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha katika maeneo kadhaa ya nchi hiyo, na kulazimisha familia nyingi kuhama makazi yao.

Mafuriko ya Kenya pia yameharibu miundo mbinu mbalimbali nchini humo.

Huduma ya Taifa ya Polisi Kenya imeeleza kuwa maporomoko ya matope yameripotiwa katika kaunti za Tharaka Nithi, Elgeyo-Marakwet na Kiambu, ambapo nyumba zimeharibiwa na kaya kulazimika kuhama makazi kufuatia siku kadhaa za mvua zinazoendelea kunyesha.

Wafanyakazi wa huduma za ukokoaji kutoka mashirika mbalimbali wametumwa katika maeneo yaliyoathiriwa na maporomoko ya udongo kuendeleza shughuli za uokoaji, kuwahamisha watu kutoka maeneo hatari na kusambaza misaada ya dharura. 

Maafisa husika wa Kenya wamesema kuwa juhudi pia zinaendelea kubaini maeneo hatarishi ili kuzuia maafa zaidi.

Mvua zinazoendelea kunyesha ni sehemu ya msimu wa mvua kubwa zinazoendelea kushuhudiwa Kenya, ambao kwa kawaida huanza mwezi Machi hadi Mei; na mara nyingi huambatana na mafuriko na maporomoko ya udongo hasa katika maeneo ya miinuko na mijini yenye mifereji duni ya maji.