Pars Today
Hatimaye Profesa Abraham Kithure Kindiki ameapishwa kuwa Naibu Rais mpya wa Kenya, kuja kurithi mikoba ya Rigathi Gachagua ambaye alibanduliwa mamlakani na Bunge la nchi hiyo mwezi uliopita wa Oktoba.
Baadhi ya vyombo vya habari vya Kenya vimeripoi kuwa, siasa za madai ya usaliti na njama za watu kuuawa zimeanza kujitokeza tena nchini humo baada ya naibu rais aliyetimuliwa mamlakani kudai alijaribiwa kulishwa sumu mara mbili.
Rais William Ruto wa Kenya ameiomba Mahakama Kuu kutupilia mbali kesi kadhaa za kupinga kuondolewa madarakani Rigathi Gachagua kama Naibu Rais, akisema kuwa masuala yaliyoibuliwa katika kesi hizo yametengewa Mahakama ya Juu pekee.
Naibu Rais wa Kenya aliyetimuliwa, Rigathi Gachagua amedai kujiri majaribio mawili yaliyofeli ya kutaka kumuua mwezi Agosti na Septemba mwaka huu.
Mahakama Kuu nchini Kenya leo imetoa amri ya muda ya kusimamisha kubadilishwa kwa Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua.
Waziri wa mazingira na maliasili wa Kenya, Aden Duale amesema kuwa serikali itaendeleza mpango wake wa kuwahamisha watu wanaoishi kando kando ya mito nchini humo.
Bunge la Kitaifa la Kenya limepasisha kwa wingi wa kura hoja ya kumng’oa madarakani Naibu Rais wa nchi hiyo, Rigathi Gachagua.
Watu wasiopungua tisa wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati mgodi usio rasmi wa dhahabu ulipoporomoka na kuwaangukia wachimba dhahabu hao huko kaskazini mwa Kenya karibu na mpaka wa Ethiopia.
Kaimu Mkuu wa Polisi nchini Kenya Ijumaa ya jana alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela baada ya kukaidi mara kwa mara amri ya kutoa ushahidi kuhusu mahali walipo watu watatu ambao wametoweka baada ya kudaiwa kukamatwa na maafisa wa polisi.
Raia wa Kenya aliyekiri kuhusika na mauaji ya wanawake 42 ambao baadhi yao miili yao ilipatikana imetupwa katika eneo la kutupa taka jijini Nairobi, ametoroka gerezani.