John Mearsheimer: Vita dhidi ya Iran ni kushindwa mutlaki Marekani
-
John Mearsheimer
Mnadharia wa mahusiano ya kimataifa wa Marekani, John Mearsheimer, amevitaja vita dhidi ya Iran kuwa ni kosa lenye janga kubwa zaidi katika historia ya sera za kigeni na kushindwa kabisa kwa Marekani.
John Mearsheimer amesema kwamba: Vita vya Marekani dhidi ya Iran, vimetimulia kivumbi vita vya Iraq, na sasa vitarekodiwa kama kosa kubwa zaidi katika historia ya sera za kigeni za Marekani.
Amesema: Trump anataka kukomesha vita, lakini njia pekee ya kuvizuia ni kujisalimisha na kukubali kushindwa. Hakuna njia ya kujiokoa kutoka kwenye hali hii. Ameongeza kwa kusema: "Vita dhidi ya Iran ni janga kubwa, kwa hivyo tunalazimika kufanya makubaliano ambayo yanainufaisha Iran."
Wakati huo huo, ripoti ya CNN imesema karibu asilimia 80 ya Wamarekani wanamlaumu Rais wa nchi hiyo, Donald Trump, kwa ongezeko la bei ya petroli. Pia, kura ya maoni ya Washington Post, ABC News na Ipsos inaonyesha kuwa, Wamarekani hawaridhishwi kabisa na utendaji wa rais wao kuhusu vita dhidi ya Iran na masuala mengine muhimu.