Kongo: Mkurugenzi Mkuu wa WHO atahadharisha kuhusu mlipuko wa Ebola
-
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dr Tedros Adhanom
Baada ya kurejea kutoka ziarani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ametahadharisha kuhusu mlipuko wa Ebola.
Akiwa Kongo, Tedros Adhanom Gebreyesus alikutana na Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi na kumpongeza kwa jitihada zake za kupambana na mlipuko huo.
Hata hivyo hadi sasa, anasema haitoshi: Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola rekodi za kutia wasiwasi.
Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amebainisha kuwa na hapa ninamnukuu: "Tayari huu ni mlipuko wa pili kwa ukubwa wa Ebola kuwahi kurekodiwa, na unaenea kwa kasi zaidi kuliko mlipuko wowote wa awali wa ugonjwa wa Ebola. Kwa kasi yake ya sasa, unaelekea kuuzidi mlipuko wa Ebola uliotokea Afrika Magharibi kati ya mwaka 2014 na 2016. Rasmi, maambukizi 4,449 yamethibitishwa, huku vifo 2,061 vikisajiliwa katika majimbo matano na maeneo 53 ya afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo."
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani pia amebainisha wasiwasi wake kwamba vifo vinatokea pia katika maeneo ambayo hayana vituo vya matibabu. Amesema, hii inamaanisha kuwa ni vigumu sana kuwafuatilia watu waliotangamana na wagonjwa katika maeneo hayo.
“Jambo la kutia wasiwasi zaidi ni kwamba tunashuuhdia idadi kubwa ya vifo vikitokea katika jamii badala ya katika vituo vya matibabu, na vifo hivyo vinahusisha watu ambao hawamo kwenye orodha zinazojulikana za waliotangamana na wagonjwa. Hii inaashiria kuwepo kwa minyororo ya maambukizi tusiyoifahamu; na hatutaweza kukomesha mlipuko huu hadi pale tutakapobaini na kukata kukata kila mnyororo wa maambukizi,"amesema Dakta Tedros.