Hifadhi ya makombora ya Marekani yaathiriwa pakubwa na vita vya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141324-hifadhi_ya_makombora_ya_marekani_yaathiriwa_pakubwa_na_vita_vya_iran
Vita na Iran vimepunguza pakubwa akiba ya makombora ya Marekani na kuibua vizuizi katika uzalishaji katika sekta ya ulinzi huku Washington ikilazimika Washington kupima uwezo wake wa kuhuisha upya akiba ya makombora ili kuwa tayari kukabiliana na migogoro mingine.
(last modified 2026-09-09T11:07:49+00:00 )
Sep 09, 2026 11:05 UTC
  • Vita vya Iran na kupungua makombora ya US
    Vita vya Iran na kupungua makombora ya US

Vita na Iran vimepunguza pakubwa akiba ya makombora ya Marekani na kuibua vizuizi katika uzalishaji katika sekta ya ulinzi huku Washington ikilazimika Washington kupima uwezo wake wa kuhuisha upya akiba ya makombora ili kuwa tayari kukabiliana na migogoro mingine.

Vita haviwezi kupimwa kwa kuzingatia tu idadi ya mashambulizi, makombora yaliyofyatuliwa, au maeneo yaliyotekwa katika uwanja wa vita. Moja ya vigezo muhimu zaidi ni gharama zinazosababishwa na vita na kuathiri nguvu ya kijeshi, uchumi, na uwezo wa kuzuia uchokozi wa pande husika; gharama ambazo wakati mwingine hudhihirisha athari zake miezi au hata miaka kadhaa baada ya kumalizika mgogoro.

Ni katika muktadha huu ambapo ripoti ya hivi karibuni ya gazeti la Los Angeles Times kuhusu hali ya akiba ya makombora ya Marekani baada ya vita dhidi ya Iran inapata umuhimu wa pekee.

Ripoti hiyo, imerejelea makadirio yaliyochapishwa kuhusu akiba ya makombora ya kujilinda ya Marekani, na kubainisha kuwa Washington ilitumia sehemu kubwa ya makombora yake ya kisasa ya aina ya Patriot na THAAD wakati wa vita, na kwamba kujaza upya akiba hiyo kwa kutumia uwezo wa sasa wa sekta ya ulinzi ya Marekani kunaweza kuchukua miaka kadhaa.

Kulingana na ripoti hiyo, Marekani ilitumia takriban asilimia 60 ya akiba yake ya makombora ya kisasa ya kujilinda katika miezi mitano ya kwanza ya vita.

Makadirio ya Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS) pia yanaonyesha kuwa akiba ya Marekani ya makombora ya Patriot na THAAD duniani ilipungua kutoka takriban makombora 2,800 mwanzoni mwa vita hadi takriban 1,100 kufikia mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Takwimu hizi zinakuwa na uzito mkubwa zaidi hasa ikizingatia kwamba kasi ya uzalishaji katika sekta ya ulinzi ya Marekani iko chini sana ikilinganishwa na kiwango ambacho makombora haya hutumiwa katika vita vikubwa.