Kwa nini UAE imekariri tena madai yake kuhusu visiwa vitatu vya Iran?
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i141954-kwa_nini_uae_imekariri_tena_madai_yake_kuhusu_visiwa_vitatu_vya_iran
Katika kujibu madai ya mara kwa mara ya UAE kuhusu visiwa vitatu vya Iran, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza tena msimamo wa Tehran, akisema kuwa Abu Musa, Tunb Kubwa na Tunb Ndogo ni sehemu isiyotenganishika ya ardhi ya Iran na kwamba kuraririwa kwa madai yasiyo na msingi hakubadilishi chochote kuhusu uhalisia wa kihistoria na kisheria wa visiwa hivyo.
(last modified 2026-10-05T06:29:00+00:00 )
Oct 05, 2026 06:25 UTC
  • Kwa nini UAE imekariri tena madai yake kuhusu visiwa vitatu vya Iran?

Katika kujibu madai ya mara kwa mara ya UAE kuhusu visiwa vitatu vya Iran, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza tena msimamo wa Tehran, akisema kuwa Abu Musa, Tunb Kubwa na Tunb Ndogo ni sehemu isiyotenganishika ya ardhi ya Iran na kwamba kuraririwa kwa madai yasiyo na msingi hakubadilishi chochote kuhusu uhalisia wa kihistoria na kisheria wa visiwa hivyo.

Kazem Gharibabadi ameitaka Abu Dhabi kuzingatia kanuni za ujirani mwema na uhalisia wa kihistoria na kisheria wa eneo hili badala ya kurudiarudia madai yasiyo na msingi. Umuhimu wa msimamo huu unavuka mipaka ya mzozo wa muda mrefu wa umiliki wa ardhi pekee. UAE imewasilisha tena madai yake kuhusu visiwa vitatu vya Iran katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, wakati ambapo nafasi ya Abu Dhabi katika masuala ya usalama wa kikanda imevuka mipaka ya hadhi yake ya awali katika eneo. Kwa hakika, UAE imekuwa ikitekeleza sera za kichokozi zinazofuatiliwa na Marekani pamoja na utawala wa Kizayuni dhidi ya baadhi ya nchi. Kuanzia Yemen na Sudan hadi Libya na Pembe ya Afrika, UAE imeibuka kama mhusika mkuu katika siasa za kikanda, huku ripoti zikionyesha kuongezeka kwa nafasi yake katika migogoro ya Afrika na mchango wake katika kuchochea ukosefu wa amani na utulivu barani humo.

Sera hii ya kichochezi inazidi kupata uzito inapochunguzwa sambamba na uhusiano unaozidi kuimarika kati ya Abu Dhabi na utawala wa Kizayuni. Tangu kuanzishwa kwa Makubaliano ya Abraham mwaka 2020, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umeimarisha uhusiano wake wa kidiplomasia na kiusalama na utawala wa Kizayuni. Hivi karibuni, Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel, alikutana na rais wa UAE mjini Abu Dhabi, ambapo walijikita katika kuimarisha uhusiano wa pande mbili na kujadili hali ya mambo katika eneo, likiwemo suala la Iran. Mkutano huo unaonyesha kuwa ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili haujasimama, bali unaendelea hata katika mazingira tata ya vita katika eneo.

Kwa mtazamo wa Tehran, kipindi hiki ni chenye umuhimu mkubwa. Katika miaka ya karibuni, utawala wa Kizayuni umekuwa ukijaribu kuvuruga usalama wa Iran kwa kuimarisha ushirikiano wake wa kisiasa, kiintelijensia, na kiusalama na baadhi ya nchi za Kiarabaru za Ghuba ya Uajemi. Katika muktadha huu, upanuzi wa ushirikiano wa kiusalama kati ya Abu Dhabi na Tel Aviv, pamoja na ushiriki hai wa UAE katika migogoro ya kikanda, ni sehemu ya mwelekeo ambao umesababisha kuongezeka mashinikizo na kubadilika uwiano wa kiusalama katika maeneo jirani na Jamhuri ya Kiislamu. Suala la visiwa hivyo linapata umuhimu wa ziada ndani ya mfumo huu. Kwa upande mmoja, UAE haiwezi kudai kuheshimu mamlaka ya kujitawala na umoja wa ardhi ya mataifa huku, kwa upande mwingine, ikitumia ushirikiano wa kiusalama na pande hasimu za kigeni dhidi ya Iran. Uhusiano na ujirani mwema hauoani kabisa na madai ya mara kwa mara ya kumiliki maeneo ya ardhi ya Iran. Vilevile, ushirikiano wa kiusalama na utawala ambao ndio chanzo kikuu cha ukosefu wa usalama na uchokozi katika eneo hauwezi kuoanishwa na madai ya kutopendelea upande wowote katika migogoro ya kikanda. Hoja nyingine muhimu ni kwamba madai ya kumiliki eneo hayageuki kuwa haki ya kisheria kutokana tu na kurudiwarudiwa kisiasa. Kuundwa kwa Umoja wa Falme za Kiarabu mwaka 1971, na kuendana kwa jambo hilo na matukio yanayohusu visiwa hivyo, hakumaanishi hata kidogo kwamba Abu Dhabi ilipata mamlaka ya umiliki wa moja kwa moja wa visiwa hivyo. Iran iliimarisha mamlaka yake juu ya visiwa hivyo katika kipindi hicho hicho, ambapo mkataba wa maelewano kuhusu kisiwa cha Abu Musa ulitiwa saini kati ya Iran na Sharjah mwaka 1971. Hivyo, jitihada za kubadilisha madai ya kisiasa kuwa "uhalisia wa kisheria" kwa kuyakariri mara kwa mara katika Umoja wa Mataifa hazina msingi wowote wa kisheria.

Iran haipingi kuwa na ushirikiano na ijirani mwema na majirani zake, lakini haitafanya umoja wa ardhi yake kuwa suala la majadiliano ya kisiasa. Sera yoyote ya kikanda inayolenga kudhoofisha usalama wa Iran, iwe ni kupitia ushirikiano wa kiusalama au madai ya kumiliki ardhi, itakabiliwa na hatua madhubuti za Iran. Mbali na hayo, njia ya kufikia utulivu wa kweli katika Ghuba ya Uajemi haipo katika miungano na madola ya nje ya eneo au utawala wa Kizayuni, bali katika kuheshimiana kwa ajili ya kulinda mamlaka, umoja wa ardhi na usalama wa mataifa ya eneo hili.