-
WHO: Maambukizi ya Ebola yanapungua katika jimbo la Ituri lililoathirika vibaya nchini DRC
Sep 17, 2026 11:53Usambazaji wa virusi vya Ebola unapungua katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Ituri lililoathirika vibaya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.
-
Mapigano yazuka kati ya Polisi DRC na waandamanaji wanaopinga mabadiliko ya Katiba
Sep 17, 2026 02:47Mamia ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameingia mitaani kupinga mabadiliko ya Katiba, ambayo kwa mujibu wa wapinzani yanaweza kufungua njia ya kuongezwa muda wa rais kuweko madarakani. Polisi walitumia mabomu ya machozi na kufyatua risasi hewani katika jaribio la kuwatawanya waandamanaji.
-
Mlipuko wa Ebola DRC wavuka kiwango cha wagonjwa 7,000 na kuenea hadi mkoa wa saba
Sep 13, 2026 07:18Ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) umevuka kiwango cha wagonjwa 7,000 waliothibitishwa na kufikia mkoa wa saba baada ya mgonjwa wa kwanza kugundulika katika mkoa wa Sud-Ubangi.
-
WHO: Vituo vya Ebola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimezidiwa
Sep 10, 2026 02:47Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, vituo vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo vimeelemewa kutokana na kuongezeka idadi ya maambukizi ya ugonjwa huuo.
-
Kongo yaimarisha udhibiti wa serikali kwa data za uchimbaji madini
Sep 08, 2026 11:00Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa inaratibu mpango wa kuimarisha udhibiti wa serikali kwa data ya kijiolojia ili kuboresha mapato ya mabilioni ya dola katika sekta ya uchimbaji madini kwa lengo la kusimamia pakubwa maendeleo ya utajiri mkubwa wa madini wa nchi hiyo.
-
Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha moto uliosababisha vifo vya watu 22 harusini, Kinshasa
Sep 06, 2026 11:29Mamlaka husika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeanzisha uchunguzi kuhusu moto uliotokea kwenye sherehe ya harusi jijini Kinshasa na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 22.
-
Upinzani DRC wamtaka Tshisekedi kuachana na mpango wa kubadili katiba
Aug 25, 2026 11:26Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amemtaka Rais Felix Tshisekedi kuachana na mapendekezo ya kufanyia marekebisho katiba ambayo wapinzani wanahofia yanaweza kutoa mwanya kwa rais huyo kugombea muhula wa tatu wa urais.
-
Rais wa zamani wa Kongo, Joseph Kabila, apinga vikwazo vya US mahakamani
Aug 23, 2026 13:54Katika kesi iliyofanyika mahakamani huko Washington, Joseph Kabila ambaye aliongoza Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia 2001 hadi 2019 ametaka jina lake liondolewe kwenye orodha nyeusi ya Wizara ya Fedha ya Marekani.
-
UN yaonya: Mlipuko wa Ebola nchini DR Congo 'unaongezeka kwa kasi' baada ya zaidi ya watu 2,500 kuaga dunia
Aug 22, 2026 03:29Umoja wa Mataifa ulitangaza jana Ijumaa kwamba virusi vya Ebola vinaenea kwa kasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya kuua zaidi ya watu 2,500, ukitoa wito wa kutolewa misaada zaidi na kuonya kwamba ufadhili uliotolewa hadi sasa utaisha ndani ya wiki chache.
-
Matumaini baada ya DRC kupokea dozi 70,000 za chanjo ya Ebola
Aug 21, 2026 10:22Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, na Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, Africa CDC, zimekaribisha uamuzi wa kuipatia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, dozi 70,000 za chanjo ya Ervebo ili kuimarisha mapambano dhidi ya mlipuko wa Ebola aina ya Bundibugyo.