Al Burhan awataka Wasudan wote wabebe silaha dhidi ya RSF
Nov 15, 2025 04:23 UTC
Mkuu w Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al Burhan amemtaka kila Msudan abebe silaha kupambana na waasi wa RSF akisisitiza kwamba hakutakuwa na mapatano na waasi hao.
Amewataka Wasudan wote kushiriki katika kile alichokiita "vita vya utu na heshima," akitoa mwito kwa "yeyote anayeweza kubeba silaha" kujiunga na mapambano dhidi ya RSF.
Jenerali Al-Burhan amesisitiza pia kwamba watu wa Sudan hawatokubali kutawaliwa na RSF au wafuasi wake, akitoa mwito kwa jamii ya kimataifa kukusanya silaha kutoka kwa makundi hayo na kuleta amani ya kudumu nchini Sudan.