Hamas yaonya kuhusu kuongezeka janga la kibinadamu Ukanda wa Gaza
-
Hamas yaonya kuhusu kuongezeka janga la kibinadamu Gaza
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imeonya kuhusiana na kushadidi janga la kibinadamuu katika Ukanda wa Gaza.
Onyo hilo limetolewa na msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ambaye ametahadharisha kuhusu kushadidi maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kufuatia mvua zilizonyesha hivi karibuni.
Siku ya Jumamosi, msemaji wa Hamas Hazem Qassem alitoa wito wa kuwepo kwa msimamo wa mara moja na madhubuti wa taasisi za kimataifa za Kiislamu na Kiarabu, akielezaa kuzidi kwa hali isiyovumilika katika Ukanda wa Gaza baada ya mvua za hivi karibuni.
Msemaji wa Hamas anaonya kwamba maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza yamechukua mwelekeo mbaya zaidi sambamba na kuwadia majira ya baridi; hali hii inahitaji uchukuaji hatuua za wazi na za haraka kutoka kwa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu kwa kuzingatia nyaraka za uanzilishi wa taasisi hizi.