Iran yapinga na kuyatoa maanani madai ya kundi la G7 dhidi yake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i133148-iran_yapinga_na_kuyatoa_maanani_madai_ya_kundi_la_g7_dhidi_yake
Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, madai yaliyomo kwenye taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazounda G7 uliofanyika nchini Canada kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayana msingi wala nadhari na hayakubaliki.
(last modified 2025-11-14T05:59:04+00:00 )
Nov 14, 2025 03:22 UTC
  • Iran yapinga na kuyatoa maanani madai ya kundi la G7 dhidi yake

Esmail Baghaei, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, madai yaliyomo kwenye taarifa iliyotolewa mwishoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zinazounda G7 uliofanyika nchini Canada kuhusu Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayana msingi wala nadhari na hayakubaliki.

Baghaei amebainisha kuwa, kurudiwa msimamo usio na nadhari na uwajibikaji wa nchi wanachama wa G7 wa kuidhinisha hatua haramu na isiyo na msingi iliyochukuliwa na nchi tatu za Ulaya na Marekani ya kutumia vibaya utaratibu wa utatuzi wa tofauti zinazozuka kwenye makubaliano ya JCPOA ili kurejesha dhidi ya Iran maazimio ya Baraza la Usalama yaliyokwishafutwa, ni sawa na kuunga mkono hatua inayokhalifu sheria za kimataifa, na akasisitiza kwamba msimamo huo uliochukuliwa na G7 hauondoi kwa namna yoyote ile asili ya kutokuwa na uhalali wa kisheria na kutokubalika hatua ya nchi hizo tatu za Ulaya na Marekani.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha uchokozi na uvamizi wa kijeshi uliofanywa kinyume cha sheria na utawala za Kizayuni na Marekani dhidi ya Iran wa kuvishambulia vituo vyake vya miradi ya nyuklia inayoendeshwa kwa malengo ya amani; na akasema, hatua ya G7 ya kuitolea wito Iran wa kuitaka itoe ushirikiano kwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki pasi na kuashiria chochote kuhusu jinai ya pamoja iliyofanywa na Marekani na utawala wa kizayuni ni ya kinafiki na uingiliaji wa masuala ya taifa hili.

Baghaei amesisitiza kwa kusema: "kimsingi, Marekani ndiye msababishaji mkuu wa hali ya sasa kutokana na kujiondoa kinyume cha sheria na kwa upande mmoja katika JCPOA mwaka 2018 na kwa kuvishambulia kijeshi vituo vya miradi ya amani ya nyuklia vya Iran; na kwa hatua zilizochukua nchi hizo tatu za Ulaya ya kuitii Marekani na kushindwa kutimiza majukumu yao, pamoja na kuunga mkono uchokozi wa kijeshi wa Marekani na utawala wa Kizayuni dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, sio tu zimekiuka waziwazi majukumu ziliyonayo katika JCPOA, lakini pia zimedhihirisha wazi nia mbaya ziliyonayo kwa kupuuza mipango na juhudi zote ilizofanya Iran kwa ajili ya kuendeleza diplomasia.../