Rais Pezeshkian asifu unyenyekevu wa Kiongozi Muadhamu
Rais Masoud Pezeshkian amesimulia kwa kina mkutano wake wa hivi karibuni na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei, akielezea hali ya kikao hicho pamoja na sifa za binafsi, kimaadili na kiuongozi alizozishuhudia kwa Kiongozi huyo.
Rais Pezeshkian amesema mkutano huo ulifanyika katika mazingira ya ukarimu na uaminifu na kuendelea kwa takriban masaa mawili na nusu.
Kwa mujibu wa Rais Pezeshkian, kilichojitokeza zaidi kuliko jambo lolote ni mtazamo wa unyenyekevu, uaminifu wa dhati na heshima ya hali ya juu wa Kiongozi Muadhamu, mwenendo uliogeuza kikao hicho kuwa majadiliano yaliyojengwa juu ya imani, utulivu, kuelewana na mazungumzo ya wazi ya moja kwa moja.
Rais Pezeshkian amesisitiza pia umuhimu wa kuimarisha mshikamano, kuaminiana na huruma katika ngazi zote za usimamizi wa serikali na utawala wa nchi.
Amebainisha kuwa pale kiongozi wa juu kabisa wa taifa anaposhirikiana na maafisa na wananchi kwa maadili ya hali ya juu, unyenyekevu na roho ya kuwajali watu, mwenendo huo huwa mfano wa kuigwa katika mfumo mzima wa utawala na uongozi wa nchi.
Mfumo huo, aliongeza, unajengwa juu ya uwajibikaji, ukaribu na wananchi, na kusikiliza kwa dhati changamoto na mahitaji yao, sambamba na mwenendo na misingi ya Kiongozi muadhamu aliyeuawa shahidi.
Ayatullah Seyyed Mojtaba Khamenei alichaguliwa kuwa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu muda mfupi baada ya kuuawa kwa baba yake na mtangulizi wake, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, ambaye aliuawa katika kama shambulio la kigaidi lililofanywa na Marekani na Israel mnamo Februari
28.