Russia: Tumejiweka tayari kikamilifu kukabiliana na vitisho vya kijeshi vya Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/world-i133142-russia_tumejiweka_tayari_kikamilifu_kukabiliana_na_vitisho_vya_kijeshi_vya_magharibi
Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema, Moscow ina uelewa kamili kwamba nchi za Magharibi zinajizatiti upya kijeshi kwa makabiliano zinayoweza kuanzisha dhidi Russia, na kwamba Moscow nayo imeshajiweka tayari kikamilifu kwa sinario kama hiyo.
(last modified 2026-01-05T06:17:05+00:00 )
Nov 14, 2025 02:33 UTC
  • Dmitry Peskov
    Dmitry Peskov

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin, Dmitry Peskov amesema, Moscow ina uelewa kamili kwamba nchi za Magharibi zinajizatiti upya kijeshi kwa makabiliano zinayoweza kuanzisha dhidi Russia, na kwamba Moscow nayo imeshajiweka tayari kikamilifu kwa sinario kama hiyo.

Peskov ameeleza kuwa, anakubaliana na Rais wa Serbia Aleksandar Vucic, ambaye alionya mapema wiki hii kwamba kujizatiti kijeshi Ulaya kunakofanywa kwa kasi kunazidisha uwezekano wa kuzuka mzozo wa moja kwa moja kati ya Russia na mataifa ya Magharibi.

"Kuna hisia za wazi (za kijeshi katika nchi za Magharibi), na hicho ni kitu kibaya," ameeleza Peskov na kuongezea kwa kusema: "lakini siku zote tumekuwa tukijua kwamba hatari hii ipo na tumeshachukua mapema hatua zote za lazima ili kulinda maslahi na usalama wetu."

Mpango wa Umoja wa Ulaya wa kujizatiti tena kwa zana za kivita, unaojumuisha pendekezo la kutumia mabilioni ya yuro, unahalalishwa kwa kisingizio cha kuwepo kitisho cha Russia. Moscow, hata hivyo inasisistiza kuwa, madai hayo yametungwa ili kuzibabaisha fikra za umma zisishughulishwe na matatizo ya kiuchumi na manung’uniko ya kijamii yanayoikabili jumuiya hiyo.

“Wanazitesa nafsi zao kwa kuongeza zaidi bajeti za kijeshi," amesema Peskov na kuongezea: "Poland tayari imeshaongeza matumizi yake ya kiulinzi hadi karibu 5% ya Pato la Taifa, na wengine wanafuata njia hiyo hiyo, japokuwa wanaua chumi zao wenyewe kwa kufanya hivyo."

Moscow inakuchulia kujipanua kunakoendelea kufanywa na shirika la kijeshi la NATO kuelekea mashariki na sera za makabiliano za Magharibi kuwa ndio chanzo kikuu cha mzozo wa Ukraine na hali mbaya ya sasa ya kiusalama ya Ulaya. Katika mkutano wake wa mwaka 2008 uliofanyika mjini Bucharest, Romania kambi hiyo ya kijeshi inayoongozwa na Marekani iliahidi kuikubali Ukraine iwe mwanachama wake mpya. Kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2014 nchini Ukraine ambayo yaliungwa mkono na nchi za Magharibi, nchi hiyo  ilipitisha sera ya wazi ya uadui dhidi ya Russia…/