Baqaei: Vikosi vya Iran viko macho kukabiliana na vitisho vyovyote vya adui
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135182-baqaei_vikosi_vya_iran_viko_macho_kukabiliana_na_vitisho_vyovyote_vya_adui
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kuhusu mazingira yaliyozushwa ya kuonesha kuna uwezekano wa kurudiwa uchokozi wa kijeshi dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa: Kilicho muhimu na kinachotuhusu sisi ni kuimarisha nguvu zetu na kuwa macho zaidi kulihami taifa la Iran.
(last modified 2026-01-06T08:41:19+00:00 )
Jan 06, 2026 08:41 UTC
  • Baqaei: Vikosi vya Iran viko macho kukabiliana na vitisho vyovyote vya adui

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kuhusu mazingira yaliyozushwa ya kuonesha kuna uwezekano wa kurudiwa uchokozi wa kijeshi dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa: Kilicho muhimu na kinachotuhusu sisi ni kuimarisha nguvu zetu na kuwa macho zaidi kulihami taifa la Iran.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmail Baqaei, amesema kuwa, mwaka jana 2025 ulikuwa mwaka mbaya zaidi katika suala la kutoheshimiwa sheria za kimataifa... Kile tulichokishuhudia Ghaza na ambacho kwa bahati mbaya, bado kinaendelea katika Ukingo wa Magharibi, ni mfano wa wazi wa kutumia aina mbaya mabavu kulidhibiti eneo hili.

Baqaei amesema kuwa, mwaka 2025, tulishuhudia ukiukwaji wa wazi wa sheria za kimataifa na bila ya shaka yoyote jinai ya Marekani ya kushambulia la vituo vya nyuklia vya matumizi ya amani vya Iran ni ukiukwaji wa wazi wa uhuru wa kitaifa. Licha ya uchungu wote tulioushuhudia mwaka wa 2025 na ambao ulimwengu pia uliuhisi kivitendo, lakini nina natumai kwamba 2026 utakuwa mwaka wa kukomeshwa uhalalishaji wa vitendo vya kihalifu na uvunjaji sheria.

Aidha amejibu swali kuhusu kuhamishwa Kituo cha Ain al-Assad nchini Iraq na vikosi vya Marekani na uwezekano wa kuweko uhusiano kati ya matukio hayo kufanyika uchokozi mpya dhidi ya Iran akisema kwamba Iran imejiandaa kikamilifu kujilinda lakini pia maafisa wakuu wa Iraq wamesema kwamba, suala hili liko ndani ya mfumo wa makubaliano yaliyopo kati ya Iraq na Marekani na kwamba serikali ya Iraq ilitakiwa tangu zamani kuchukua kituo cha Ain al-Assad mwaka huu wa 2026.