-
Rais wa Iran azitaka IMF na Benki ya Dunia kutekeleza majukumu yake ipasavyo
Apr 08, 2020 08:46Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia zinapaswa kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kwamba, katika mazingira magumu ya sasa kama hayatotekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa, basi walimwengu watakuwa na ufahamu na uelewa mwingine kuhusiana na jambo hilo.
-
Kuanza awamu mpya ya ustawi wa pande zote na wa kujivunia wa Taasisi ya Nishati ya Nyuklia ya Iran
Apr 08, 2020 07:28Dk Ali Akbar Salehi, Mkuu wa Taasisi ya Nishati ya Atomiki ya Iran alisema jana Jumanne kwa mnasaba wa maadhimisho ya tarehe 8 Aprili, Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia nchini Iran kwamba awamu mpya ya ustawi wa pande zote na wa kujivunia imeanza katika taasisi hiyo.
-
Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia ya Iran yaadhimishwa nchini
Apr 08, 2020 03:37Leo Jumatano tarehe 8 Aprili sawa na tarehe 20 Farvardin imepewa jina la "Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia" katika kutambua jitihada za kujivunia za wasomi wa nyuklia wa Iran katika kukamilisha mzunguko wa utengenezaji wa fueli ya nyuklia.
-
Zarif: Iran haihitaji sadaka ya Trump; Marekani iache kuzuia uuzaji wa mafuta ya Iran
Apr 07, 2020 19:11Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haina haja na sadaka ya serikali ya Marekani na kusisitiza udharura wa kuondolewa vikwazo vya Washington dhidi ya Tehran.
-
Mazungumzo ya simu ya Marais wa Iran na Ufaransa; sisitizo juu ya udharura wa kusitishwa vita vya kiuchumi dhidi ya Iran
Apr 07, 2020 19:02Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alasiri ya juzi Jumatatu Aprili 6 alifanya mazungumzo kwa njia ya simu na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, ambapo sambamba na kukaribisha kwa mikono miwili ubinifu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kutangaza kusitishwa vita katika maeneo mbalimbali ya dunia katika kipindi hiki cha virusi vya Corona amesema kuwa, ana matumaini ubunifu huo utamujuisha pia vita vya kiuchumi dhidi ya Iran.
-
Waziri wa Afya: Iran imeshafikia hatua ya kuuweza ugonjwa wa corona
Apr 07, 2020 10:28Waziri wa Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu wa Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu imefikia hatua ya kuuweza ugonjwa wa corona na akaongeza kwamba, katika siku zijazo baadhi ya mikoa nchini itakuwa imeshafikia kwenye awamu ya kuudhibiti ugonjwa huo.
-
Kuendelea kutolewa miito ya kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran
Apr 07, 2020 06:53Kuibuka virusi vya Corona ulimwenguni kumeyafanya mataifa yote ya dunia si tu kwamba, yatumie uwezo wao wa ndani katika sekta ya afya na tiba, bali mataifa hayo sambamba na kutilia mkazo juu ya ulazima wa kuweko ushirikiano wa dunia nzima kwa ajili ya kudhamini mahitaji ya kukabiliana na virusi vya Corona yanafanya hima pia ya kuchukuliwa hatua za kukabiliana na maradhi hayo sambamba na kuwatibu waathiwa wa virusi hivyo katika mataifa mengine.
-
Mgogoro wa corona umedhihirisha kuwa US haiwezi hata kujiongoza yenyewe
Apr 07, 2020 03:04Msaidizi Maalumu wa Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) katika masuala ya kimataifa amesema mgogoro wa ugonjwa wa Covid-19 (corona) umeudhihirishia ulimwengu kuwa, utawala wa kibeberu wa Marekani ambao unajiona kuwa kiongozi na mtawala wa dunia umeshindwa hata kujiongoza wenyewe.
-
Rais Rouhani: Kuzinduliwa INSTEX ni hatua chanya, lakini haitoshi
Apr 06, 2020 23:01Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza kuzinduliwa mfumo maalumu wa mabadilishano ya fedha kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Umoja wa Ulaya (INSTEX) na kusisitiza kuwa hatua hiyo ni chanya, lakini haitoshi kukidhi maslahi yote ya Iran.
-
Zaidi ya watu 24,000 wapata afueni ya corona nchini Iran
Apr 06, 2020 09:04Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Matibabu ya Iran imetangaza kuwa, kasi ya mchakato wa kuzidi kupata afya njema na afueni kutokana na corona imeongezeka sana humu nchini kiasi kwamba hadi leo mchana watu 24 elfu na 236 walisharuhusiwa kurudi nyumbani kutoka mahospitalini baada ya kupata nafuu kikamilifu.