-
Mousavi: Serikali na taifa la Iran halina imani kabisa na maneno ya viongozi wa Marekani
Apr 06, 2020 08:58Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa, taifa na serikali ya Jamhuri ya Kiislamu haina imani kabisa na maneno ya viongozi wa Marekani na kusisitiza kuwa, Tehran haijawahi hata mara moja kuiomba Marekani iitumie misaada ya tiba na matibabu.
-
Kukabiliana na corona; kubadilisha tishio kuwa fursa
Apr 06, 2020 07:31'Nina matumaini kuhusu mafanikio ya Iran katika kukabiliana na virusi vya corona." Hiyo ni kauli ya Daktari Richard Brennan, mkuu wa ujumbe wa Shirika la Afya Duniani (WHO) uliotembelea Iran mwezi uliopita. Akizungumza na waandishi habari mjini Tehran aliongeza kuwa: "Tunawapongeza na tunajivunia wafanyakazi wa sekta ya tiba Iran kutokana na uchapakazi wao."
-
Rais Rouhani: Kazi zenye hatari ndogo ya maambukizi zinaweza kuanza Iran sambamba na kulinda sheria za afya
Apr 05, 2020 07:18Rais Hassan Rouhani was Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kazi za kiuchumi na za kati zisizo na hatari ya maambukizi ya virusi vya corona zinaweza kuanza tena hapa nchini tarehe 11 mwezi huu wa Aprili sambamba na kuchunga na kuheshumu protokali zote za afya.
-
Salehi: Wakala wa IAEA usiwe wenzo wa mashirika ya kijasusi
Apr 05, 2020 06:18Mkuu wa Shirka la Atomiki la Iran amesema kuhusu madai yaliyotolewa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ambayo sasa yanafuatiliwa na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) kwamba wakala huo haupasi kuwa wenzo unaokamilisha kazi za mashirika ya ujasusi.
-
Iran yajitosheleza katika kuzalisha vifaa vya kupambana na corona
Apr 04, 2020 22:23Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayeshughulikia masuala ya sayansi na teknolojia Daktari Sorena Sattari ametangaza habari ya kujitosheleza Iran katika uzalishaji wa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa COVID-19.
-
Mousavi: Kwa muda mrefu sasa wanadipolasia wa Marekani wamekuwa wakiwasaidia magaidi
Apr 04, 2020 22:23Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu tuhuma za kipuuzi zilizotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani dhidi ya wanadiplomasia wa Iran na kusema kuwa, kwa muda mrefu sasa wanadiplomasia wa Marekani wamekuwa wakiwapa silaha na kuwaunga mkono magaidi duniani.
-
Barua ya Iran kwa Mkurugenzi Mkuu wa WHO: Vikwazo vya Marekani ni mfano wa wazi wa jinai dhidi ya binadamu
Apr 04, 2020 22:22Kunyimwa watu haki ya kunufaika na dawa, vifaa vya matibabu na huduma za afya ni mfano wa wazi wa jinai dhidi ya binadamu
-
Iran yazindua mfumo mpya wa kupima COVID-19
Apr 04, 2020 07:09Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imezindua mfumo mpya wa kupima ugonjwa wa COVID-19 au corona. Mfumo huo unatumia Akili Bandia au Artificial Intelligence na unatumia taswira za mashine ya CT Scan kubainisha kuwepo ugonjwa wa corona katika mwili wa binadamu.
-
Maambukizi ya corona na kutoweka kwa maadili ya kibinadamu katika nchi za Magharibi
Apr 04, 2020 06:56Baada ya mlipuko wa maambukizi ya virusi vya corona katika pembe mbalimbali za dunia hivi sasa Magharibi hususan nchi za Ulaya na Marekani zimekuwa kitovu kikuu cha maambukizi ya virusi hivyo.
-
Wagonjwa takribani 18,000 wa corona wapata nafuu nchini Iran
Apr 03, 2020 09:17Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, hadi hivi sasa watu 17,935 wameshapata nafuu kikamilifu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kutoka hospitalini humu nchini.