Mousavi: Kwa muda mrefu sasa wanadipolasia wa Marekani wamekuwa wakiwasaidia magaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i60172-mousavi_kwa_muda_mrefu_sasa_wanadipolasia_wa_marekani_wamekuwa_wakiwasaidia_magaidi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu tuhuma za kipuuzi zilizotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani dhidi ya wanadiplomasia wa Iran na kusema kuwa, kwa muda mrefu sasa wanadiplomasia wa Marekani wamekuwa wakiwapa silaha na kuwaunga mkono magaidi duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 04, 2020 22:23 UTC
  • Mousavi: Kwa muda mrefu sasa wanadipolasia wa Marekani wamekuwa wakiwasaidia magaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu tuhuma za kipuuzi zilizotolewa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani dhidi ya wanadiplomasia wa Iran na kusema kuwa, kwa muda mrefu sasa wanadiplomasia wa Marekani wamekuwa wakiwapa silaha na kuwaunga mkono magaidi duniani.

Mike Pompeo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani ambaye ni maarufu kwa jina la waziri anayeeneza chuki na vita duniani, hivi karibuni alidai kuwa eti wanadiplomasia wa Iran walihusika katika mauaji fulani yaliyotokea nchini Uturuki.

Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran jana alijibu tuhma hizo za uongo na kuserma kuwa, ukweli usiopingia ni kwamba kwa muda mrefu sasa wanadiplomasia wa Marekani wamekuwa wakihusika na mapinduzi ya kijeshi, kuwapa silaha magaidi, kuchochea machafuko na chuki za kimakundi na kimadhehebu, kusaidia magenge ya magendo ya mihadarati, kuyatwenza nguvu mashirika na tawala mbalimbali, kufanya ujasusi hata dhidi ya marafiki wa Marekani, kuwasaidia maditeta pamoja na kuwapa mafunzo magaidi na vitendo vingine vingi viovu.

Mike Pompeo

 

Amesema, lakini Pompeo ambaye ni mkuu wa zamani wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA ambaye hivi sasa amevaa koti la waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo na mabwana zake wameingiza ugaidi huo katika awamu mpya yaani ugaidi wa kimatibabu na yeye mwenyewe amejaa dhambi ambazo haziwezi kufutika hata kwa kupayuka na kueneza vita kama hivi vya kisaikolojia.

Kabla ya hapo pia, Majid Takht-Ravanchi, mwakilishi wa kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa alisisitiza kuwa, hakuna mtu anayeweza kudanganywa na upayukaji na uongo wa viongozi wa Marekani kuhusu Iran.

Wakati ambapo sasa hivi dunia imezama katika kupambana na ugonjwa wa corona na unaitaka Marekani ikomeshe ugaidi wake wa kiuchumi dhidi ya Iran, Mike Pompeo amedharau yote hayo na badala yake amezuka na madai mapya ya kuwatuhumu bila sababu wanadiplomasia wa Iran kwa mambo ambayo hawakuyafanya.