Dakta Nchimbi atangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania
-
Dkt. Emmanuel Nchimbi
Dakta Nchimbi atangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais wa Tanzania
Dk Nchimbi ametoa taarifa hiyo leo Jumanne Agosti 25, 2026 nakubainisha kuwa amemwandikia barua Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kumjulisha kuhusu uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais kuanzia Septemba 4, 2026.
Katika taarifa yake, Dk Nchimbi amesema uamuzi huo umetokana na ahadi aliyompa Rais Samia wakati alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, kwamba angeendelea kumsaidia katika majukumu yake kwa uaminifu na uwezo wake wote, na angeachia nafasi hiyo iwapo angehisi Rais anahitaji mabadiliko. “Nimejiridhisha pasipo shaka kuwa Mheshimiwa Rais anatamani mabadiliko; hivyo nimeamua kutimiza ahadi yangu,” amesema Dk Nchimbi katika taarifa yake.
Aidha, amemshukuru Rais Samia pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa imani waliyoonyesha kwake, huku akiwashukuru Watanzania kwa ushirikiano na kumuunga mkono katika kipindi chake cha utumishi. Dk Nchimbi amesisitiza kuwa licha ya kustaafu siasa na utumishi wa umma, ataendelea kuwa raia mwema na kulitumikia taifa katika nafasi nyingine.