-
Mousavi: Kimya cha jamii ya kimataifa kimewahamasisha watenda jinai kuuwa raia wa Yemen
Feb 16, 2020 09:55Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulio la watenda jinai wa muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia. Shambulio hilo lilifanywa juzi usiku na wanajeshi wa Saudia Arabia na washirika wake katika mji wa al Masloub mkoani al Jawf.
-
"Njia sahihi ya kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo, ni Ulaya kufungamana na JCPOA"
Feb 16, 2020 04:37Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran inataraji kuwa nchi za Ulaya zitafungamana na ahadi zake kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kama zilizovyoahidi, na kwamba hatua hiyo ndiyo njia pekee na sahihi ya kuyapatia ufumbuzi matatizo yaliyopo.
-
Udharura wa kushikamana Waislamu, mhimili wa muqawama katika kuwafukuza wanajeshi wa Marekani Asia Magharibi
Feb 15, 2020 08:47Hii leo mhimili wa muqawama si Iran pekee bali umeenea kuanzia Bahari Nyekundu hadi ya Meditarania na kuanzia Harakati ya Ansarullah ya Yemen hadi Hizbullah ya Lebanon.
-
Zarif: Kwa ujinga na taarifa ghalati, Marekani imeisukuma Asia Magharibi kwenye ukingo wa shimo la vita
Feb 15, 2020 04:35Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amegusia jinai iliyofanywa na Marekani ya kumuua kigaidi, shahid Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds, cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH na kusisitiza kuwa, kwa ujinga wake na kwa kutegemea taarifa ghalati na zisizo sahihi, Marekani imelisukuma eneo la Asia Magharibi kwenye ukingo wa shimo la vita vikubwa.
-
Kiongozi Muadhamu: Uhimilivu mkubwa wa taifa la Iran unawastaajabisha walimwengu
Feb 15, 2020 09:57Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuhusu mahudhurio makubwa ya wananchi imara wa Iran katika maandamano ya Bahman 22, na katika kuusindikiza mwili wa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kwamba uhimilivu mkubwa wa taifa la Iran wa kuyakabili mashinikizo makubwa na ya kinyama ya Marekani umewastaajabisha wafuatiliaji wa masuala ya kimataifa.
-
Sababu za mafanikio ya Shahidi Soleimani katika mtazamo wa Sayyid Hassan Nasrullah
Feb 14, 2020 09:14Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amefanya mazungumzo na televisheni ya al Mayadeen akieleza mchango na nfasi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunda harakati hiyo ya mapambano na mafanikio ya Kamanda Qassem Soleimani.
-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa Tehran: Muamala wa Karne ni fedheha kwa Trump
Feb 14, 2020 08:36Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyosaliwa leo hapa Tehran amesema mpango wa 'Muamala wa Karne' ni fedheha kubwa na kashfa kwa Rais Donald Trump wa Marekani.
-
Salami: Shahidi Soleimani ni mhuishaji wa jihadi na shahada katika ulimwengu wa Kiislamu
Feb 14, 2020 04:17Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amemtaja Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha SEPAH kama shakhsia aliyehuisha 'harakati za jihadi na kuuawa shahidi' katika ulimwengu wa Kiislamu.
-
Kupiga hatua Iran katika sekta ya anga za mbali na kutuhumiwa kwa dhambi inayofanywa na Marekani na Ufaransa
Feb 13, 2020 23:08Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema: Suala la kurusha satalaiti na roketi la kubebea satalaiti hiyo katika anga za mbali ni jambo linalojulikana wazi duniani, wala halina uhusiano wowote na mjadala unaohusu makombora.
-
Marasimu ya maombolezo ya 40 ya shahidi Luteni Jenerali Soleimani yafanyika kote nchini Iran
Feb 13, 2020 10:06Marasimu ya maombolezo ya arubaini ya shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Qods cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ( SEPAH) yamefanyika leo kote nchini Iran kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa matabaka mbalimbali ya wananchi.