-
Iran: Muamala wa Karne ni "amani ya kutwisha na kuziuza ardhi za Palestina"
Feb 03, 2020 08:58Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njia pekee ya kuiondoa Palestina katika mkwamo wa miaka 70 ni kurejea katika kura za uma kuhusiana na hatima ya taifa la Palestina na kwamba, Muamala wa Karne ni amani ya kutwisha na kuuza ardhi za Palestina.
-
Mkuu mpya wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya yuko safarini Iran
Feb 03, 2020 08:16Josep Borell, mkuu mpya wa sera za kigeni katika Umoja wa Ulaya leo Jumanne amewasili Iran ikiwa ni safari yake ya kwanza humu nchini baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
-
Iran na Uturuki zahimiza kususiwa kikamilifu "Muamala wa Karne"
Feb 03, 2020 04:45Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki wametilia mkazo msimamo imara wa ulimwengu wa Kiislamu wa kususia kikamilifu mpango wa Kimarekani-Kizayuni uliopachikwa jina la "Muamala wa Karne."
-
Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya awasili mjini Tehran
Feb 03, 2020 04:45Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amewasili mapema leo asubuhi hapa mjini Tehran kwa ajili ya kufanya mazungumzo na viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Rouhani: Muamala wa Karne ni muamala wa fedheha na chuki
Feb 02, 2020 04:08Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameutaja 'Muamala wa Karne' kama mpango wa Marekani wa kufedhehesha, aibu na wenye kuchukiza.
-
Mkuu mpya wa Sera za Kigeni wa EU kuitembelea Iran kwa mara ya kwanza
Feb 02, 2020 03:55Mkuu mpya wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya anatazamiwa kuwasili hapa mjini Tehran kesho Jumatatu, kujadili masuala yenye umuhimu kwa pande mbili na maafisa wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
IRGC: 'Majeraha ya Ubongo' ni njia ya kuficha idadi ya askari wa Marekani waliouawa katika hujuma ya makombora ya Iran
Feb 01, 2020 10:08Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema madai ya Marekani kuhusu idadi kubwa ya wanajeshi wake waliopata 'majeraha ya ubongo' kufuatia makombora ya Iran ya ulipizaji kisasi yaliyolenga kituo cha kijeshi cha Ain al Assad nchini Iraq ni njia ya kuficha idadi ya wanajeshi waliouawa katika oparesheni hiyo.
-
'Jeshi la nchi kavu la Iran ni la tano kwa uwezo mkubwa duniani'
Feb 01, 2020 08:52Kamanda wa Jeshi la Nchi Kavu la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uwezo wa kujihami wa Iran na kusema: "Jeshi la nchi kavu la Iran ni la tano kwa uwezo wa nchi kavu duniani."
-
Bahman 12; Kuanza maadhimisho ya Alfajiri Kumi; dhihirisho la umoja na mshikamano wa taifa la Iran
Feb 01, 2020 07:47Leo Jumamosi tarehe 12 mwezi Bahman sawa na Februari Mosi ni siku ya kuanza alfajiri kumi za maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
-
Maadhimisho ya "Alfajiri Kumi" ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaanza rasmi nchini Iran
Feb 01, 2020 04:44Leo Jumamosi, tarehe 12 Bahman mwaka 1398 Hijria Shamsia inayosadifiana na tarehe Mosi Februari 2020 Miladia yameanza rasmi maadhimisho ya Alfajiri Kumi ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.