-
Timu za Iran zajitoa kwenye mashindano ya soka ya mabingwa wa Asia kulalamikia uamuzi wa kisiasa wa AFC
Jan 18, 2020 10:29Timu za Esteqhlal, Perspolis, Sepahan na Shahre-Khodroo zinazoiwakilisha Iran katika mashindano ya mabingwa wa soka wa Asia katika mwaka huu wa 2020 zimeamua kujitoa kwenye mashindano hayo kulalamikia uamuzi wa kisiasa uliochukuliwa na Shirikisho la Soka la Asia (AFC) wa kuzitaka timu hizo zicheze michezo yao yote katika nchi ngeni ya tatu.
-
Njama za Marekani za kutaka kuficha hasara kubwa za shambulizi la makombora ya Iran huko Ainul Asad
Jan 18, 2020 09:13Katika jitihada zake za kutimiza ahadi ya kulipiza kisasi kikali dhidi ya Marekani kutokana na mauaji ya kigaidi yaliyofanywa na nchi hiyo dhidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani na wana jihadi wenzake, Alfajii ya Jumatano tarehe 8 Januari Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilishambulia kambi kubwa zaidi ya wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ya Ainul Asad.
-
Hotuba za Kiongozi Muadhamu Katika Sala ya Ijumaa Tehran; ubainishaji wa nguvu na adhama ya Iran
Jan 18, 2020 04:23Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika hotuba zake za Sala ya Ijumaa wiki hii mjini Tehran, alisema: "Kushiriki kimuujiza taifa la Iran katika mazishi ya shahidi mtoharifu Qassem Soleimani na wenzake na pia jibu kali la IRGC lililotolewa kwa kushambulia kituo cha Ainul Assad cha Jeshi la Marekani (nchini Iraq) ni siku mbili ambazo zinaweza kutajwa kuwa Siku za Mwenyezi Mungu (Ayamullah). Siku hizi zimejaa somo na ibra na ni za kuainisha hatima."
-
Hotuba ya Kiongozi Muadhamu katika Swala ya Ijumaa yaakisiwa sana na vyombo vya habari vya kimataifa
Jan 17, 2020 23:28Hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika Swala ya Ijumaa iliyoswaliwa jana mjini Tehran, imeakisiwa sana na vyombo vya habari vya kigeni.
-
Mamilioni ya Wairan wafanya maandamano makubwa ya kuunga mkono uwezo wa kijeshi wa nchi hii
Jan 17, 2020 10:53Mamilioni ya raia wa Iran wamefanya maandamano makubwa katika kuunga mkono uwezo wa kijeshi na umadhubuti wa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu katika kusimama imara mbele ya Marekani, maandamano ambayo yamefanyika nchi nzima baada ya Swala ya Ijumaa.
-
Russia: Wakati ndege ya Ukraine ilipoanguka, ndege sita za kivita za Marekani zilikuwa angani karibu na Iran
Jan 17, 2020 12:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wakati tukio la kuanguka kwa ndege ya abiria ya Ukraine mjini Tehran likijiri, kwa akali ndege sita za kivita za Marekani zilikuwa angani zikiruka karibu na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran na India; juhudi kwa ajili ya kutumia sarafu ya taifa na kupanua ushirikiano wa kiuchumi
Jan 17, 2020 09:02Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo mjini New Delhi na Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India na kujadili suala la kupanua ushrikiano wa kiuchumi baina ya nchi mbili na kuchukua hatua za kuondoa baadhi ya matatizo yaliyopo katika njia hiyo.
-
Maelfu ya Wairani washiriki Sala ya Ijumaa chini ya uimamu wa Kiongozi Muadhamu
Jan 17, 2020 04:27Maelfu ya wananchi Waislamu wa Iran wamekusanyika katika eneo la Musalla wa Imam Khomeini (MA) hapa jijini Tehran wakisubiri hotuba na Sala ya Ijumaa zitakazoongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Meja Jenerali Baqeri: Marekani itapata jibu kali zaidi la Iran ikiendeleza mienendo yake hasi
Jan 17, 2020 00:00Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo Marekani itaendeleza chokochoko na mienendo yake hasi dhidi ya taifa hili, basi iwe tayari kupokea jibu kali zaidi la Iran ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Jibu la nguvu la IRGC lilikuwa pigo kwa haiba ya dola kubwa la Marekani
Jan 17, 2020 09:10Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pigo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kwa adhama ya Marekani ni jambo ambalo limepelekea nchi hiyo ifedheheke na kuongeza kuwa: "Pigo hilo kubwa na lenye nguvu haliwezi kufidiwa kwa chochote na hivyo hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kuongeza vikwazo haiwezi kuondoa fedheha hiyo."