-
Russia: Wakati ndege ya Ukraine ilipoanguka, ndege sita za kivita za Marekani zilikuwa angani karibu na Iran
Jan 17, 2020 12:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, wakati tukio la kuanguka kwa ndege ya abiria ya Ukraine mjini Tehran likijiri, kwa akali ndege sita za kivita za Marekani zilikuwa angani zikiruka karibu na mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran na India; juhudi kwa ajili ya kutumia sarafu ya taifa na kupanua ushirikiano wa kiuchumi
Jan 17, 2020 09:02Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kufanya mazungumzo mjini New Delhi na Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India na kujadili suala la kupanua ushrikiano wa kiuchumi baina ya nchi mbili na kuchukua hatua za kuondoa baadhi ya matatizo yaliyopo katika njia hiyo.
-
Maelfu ya Wairani washiriki Sala ya Ijumaa chini ya uimamu wa Kiongozi Muadhamu
Jan 17, 2020 04:27Maelfu ya wananchi Waislamu wa Iran wamekusanyika katika eneo la Musalla wa Imam Khomeini (MA) hapa jijini Tehran wakisubiri hotuba na Sala ya Ijumaa zitakazoongozwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Meja Jenerali Baqeri: Marekani itapata jibu kali zaidi la Iran ikiendeleza mienendo yake hasi
Jan 17, 2020 00:00Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema iwapo Marekani itaendeleza chokochoko na mienendo yake hasi dhidi ya taifa hili, basi iwe tayari kupokea jibu kali zaidi la Iran ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Jibu la nguvu la IRGC lilikuwa pigo kwa haiba ya dola kubwa la Marekani
Jan 17, 2020 09:10Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema pigo la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) kwa adhama ya Marekani ni jambo ambalo limepelekea nchi hiyo ifedheheke na kuongeza kuwa: "Pigo hilo kubwa na lenye nguvu haliwezi kufidiwa kwa chochote na hivyo hatua ya hivi karibuni ya Marekani ya kuongeza vikwazo haiwezi kuondoa fedheha hiyo."
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Marekani imesalimu amri moja kwa moja kwa uwezo mkubwa wa Iran katika uga wa makombora
Jan 16, 2020 11:52Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia jibu kali la makombora ya nchi hii dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani, kufuatia jinai ya Washington ya kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC na kusema kuwa suala hilo limebainisha uhalisia wa uwezo mkubwa wa makombora wa taifa hili uliomfanya adui asalim amri mbele ya Iran.
-
Rais Rouhani: Taifa la Iran limekuwa imara zaidi katika kukabiliana na njama na vikwazo vya Marekani
Jan 16, 2020 07:56Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, Marekani inafuata njia ghalati kuhusu taifa la Iran. Ameongeza kuwa, taifa la Iran limezidi kuwa na nguvu na limekuwa imara zaidi mbele ya njama na vikwazo vya Marekani.
-
Zarif: Ulaya wameamua "kuitosa" JCPOA kwa kuhofia ushuru mpya wa Trump
Jan 16, 2020 07:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameandika ujumbe mkali katika mtandao wa kijamii wa Twitter kulaani udhaifu wa nchi za Ulaya mbele ya Marekani na kuandika: Nchi tatu za Ulaya zilizobakia kwenye mapatano ya nyuklia ya JCPOA zimeamua kuyatupa makubaliano hayo kwa kuhofia ushuru mpya ambao Trump ametishia kuziwekea ushuru mpya nchi za Ulaya.
-
Dakta Zarif: Madola ya Ulaya yarekebishe mwenendo wao mkabala na Iran na JCPOA
Jan 16, 2020 04:28Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, madola matatu ya Ulaya ya Ujerumani, Uingereza na Ufaransa yanapaswa kurekebisha mwenendo wao mkabala na Iran na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
-
Hizbullah: Maelfu ya Maqassim Soleimani watalipiza kisasi cha damu yake
Jan 16, 2020 04:28Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametangaza kuwa, adui asijidanganye kwamba, kwa kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani njia ya mwanamapambano huyo haitaendelea, bali maelfu ya watu mfano wake watajitokeza kulipiza kisasi cha damu yake.