-
IRGC: Iran imefanikiwa kudhibiti uwezo na nguvu za Marekani
Jan 15, 2020 23:01Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria wimbi la hivi karibuni la ushindi wa Iran dhidi ya Marekani na kusema kuwa, "Jamhuri ya Kiislamu imefanikiwa kuidhalilisha na kuzidhibiti nguvu za Marekani."
-
Sisitizo la Iran la kutoa jibu kali kwa ukiukaji wa ahadi na kwa hatua hasi za nchi tatu za Ulaya kuhusu mapatano ya JCPOA
Jan 15, 2020 23:00Sayyid Abbas Mousavi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa radiamali sambamba na nchi tatu za Ulaya kuamua kutekeleza utaratibu wa kutatua hitilafu katika mapatano ya JCPOA na kueleza kuwa hatua hiyo si ya uwajibikaji na imechukuliwa katika hali ya udhaifu.
-
Rais Rouhani: Wananchi wa Asia Magharibi wahakikishe Marekani inaondoka katika eneo
Jan 15, 2020 09:13Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuna udharura kwa wananchi wa Asia Magharibi kufanya kila wawezalo kuhakikisha kwamba, majeshi ya Marekani yanaondoka katika eneo hili.
-
Sababu zinazoifanya ziara ya Amir wa Qatar nchini Iran kuwa na umuhimu mkubwa
Jan 15, 2020 02:43Amir wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad Aal Thani, Jumapili iliyopita ya tarehe 12 Januari 2020, alifanya ziara rasmi hapa mjini Tehran. Katika ziara hiyo, Sheikh Tamim alionana na viongozi wa ngazi za juu kabisa wa Iran akiwemo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei na Rais Hassan Rouhani.
-
Zarif: Hatua ya nchi za Ulaya ya kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu JCPOA ni kosa la kiistratijia
Jan 15, 2020 01:03Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran usiku wa kuamkia leo Jumatano ameonana na Niels Anne, Waziri Mshauri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Shirikisho ya Ujerumani mjini New Delhi, India na kusema kuwa, hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuanzisha mchakato wa kutatua hitilafu ndani ya mapatano ya nyuklia ya JCPOA ni kosa la kiistratijia.
-
IRGC: Watu milioni 25 walishiriki katika shughuli ya mazishi ya Shahidi Qassem Soleimani
Jan 14, 2020 23:20Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: " Watu milioni 25 walishiriki katika shughuli ya mazishi na kuuaga mwili wa Shahidi Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha IRGC, katika miji ya Ahvaz, Mashhad, Tehran, Qom na Kerman nchini Iran."
-
Rouhani: Iran ina irada ya kustawisha ushirikiano wa pande zote na Syria
Jan 14, 2020 09:44Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran na irada ya kuimarisha na kustawisha uhusiano wa pande zote na Syria.
-
Rais Rouhani: Jopo la uchunguzi wa ajali ya ndege ya Ukraine libuniwe
Jan 14, 2020 08:34Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa mwito wa kuundwa jopo maalumu la mahakama la kuchunguza ajali ya ndege ya Ukraine iliyoua watu 176 siku chache zilizopita hapa jijini Tehran, sanjari na kuwafikisha mbele ya sheria wahusika wa ajali hiyo.
-
Zarif: Uingereza inashirikana kibubusa na Marekani katika harakati zake za kigaidi
Jan 14, 2020 04:46Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Uingereza inaifuata kipofupofu Marekani na kushiriki kibubusa katika harakati za kigaidi za Washington katika eneo la magharibi mwa Asia.
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Uungaji mkono wa Iran kwa kambi ya muqawama utaendelea kwa kasi kubwa
Jan 14, 2020 01:13Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kubainisha kwamba uungaji mkono wa nchi hii kwa kambi ya muqawama utaendelea kwa kasi kubwa, amesema kuwa katika kipindi cha ukarabati wa Syria, Tehran pia itakuwa pamoja na wananchi na serikali ya nchi hiyo ya Kiarabuu.