Hizbullah: Maelfu ya Maqassim Soleimani watalipiza kisasi cha damu yake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i58548-hizbullah_maelfu_ya_maqassim_soleimani_watalipiza_kisasi_cha_damu_yake
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametangaza kuwa, adui asijidanganye kwamba, kwa kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani njia ya mwanamapambano huyo haitaendelea, bali maelfu ya watu mfano wake watajitokeza kulipiza kisasi cha damu yake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 16, 2020 07:58 UTC
  • Hizbullah: Maelfu ya Maqassim Soleimani watalipiza kisasi cha damu yake

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ametangaza kuwa, adui asijidanganye kwamba, kwa kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani njia ya mwanamapambano huyo haitaendelea, bali maelfu ya watu mfano wake watajitokeza kulipiza kisasi cha damu yake.

Sheikh Naim Qassim amesisitiza kuwa, katika kipindi cha uhai wake, Luteni Jenerali Qassim Soleimani alipata mafanikio mengi, na moja ya matunda aliyotaka kuyafikia ni kutimuliwa wanajeshi wa Marekani katika eneo hili la Asia Magharibi.

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, kuuawa shahidi Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH) kumekuwa sababu ya kuchukuliwa uamuzi wa kuwatimua wanajeshi wa Marekani kkatikak eneo hili.

Sheikh Naim Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon

Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa Hizbullah amesema wazi kuwa, kwa kumuua Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Wamarekani walikusudia kusimamisha mpango wa kukombolewa Palestina na kuweko mamlaka ya kujitawala kwa nchi za Asia Magharibi, hata hivyo hatuua yao hiyo itapelekea kujitoleza maelfu ya Mawassim Soleimani wapya.

Itakumbukwa kuwa,  usiku wa  kuamkia Ijumaa ya Januari 3 serikali ya Marekani ilitekeleza kitendo cha kigaidi baada ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu na Abu Mahdi al-Muhandis Naibu Mkuu wa kundi la wapiganaji wa kujitolea wa Iraq (Hashdu al Shaabi).