-
Kiongozi Muadhamu amuenzi Shahidi Soleimani, asema daima alifikiria kuhuisha Muqawama
Jan 01, 2025 13:21Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesifu na kukutaja kuwa ni kwa kipekee kujitolea kwa kamanda mkuu wa Iran wa kupambana na ugaidi, Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, ambaye aliuawa mwaka 2020 akiwa pamoja na wanajihadi wenzake katika shambulio la kigaidi la ndege isiyo na rubani ya Marekani karibu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
-
Jenerali Salami: Hakuna shaka tutalipiza kisasi cha mauaji ya Shahidi Soleimani
Jan 09, 2023 04:10Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu alivunja na kusambaratisha njama za maadui wa taifa hili, na kwamba wahusika wa mauaji yake wanapaswa kufahamu kuwa lazima Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukua hatua kujibu kitendo cha kigaidi cha kumuua shahidi kamanda huyo.
-
Wananchi wa Iran wamkumbuka Jenerali Soleimani aliyeuawa kigaidi na Marekani
Jan 03, 2023 15:21Wananchi kote katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo wametoa heshima kwa shujaa wao Jenerali Haj Qassem Soleimani, kamanda maarufu duniani wa mapambano dhidi ya ugaidi ambaye aliuawa katika hujuma ya kigaidi ya Marekani mwaka 2020.
-
Baraza la Maulamaa la Nigeria: Mauaji ya Jenerali Soleimani ni jinai
Jan 02, 2023 11:29Baraza la Maulamaa wa Kiislamu Nigeria, limelaani vikali mauaji ya kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Luteni Jenerali Qassem Solaimani na kusema mauaji hayo yaliyotekelezwa na Marekani ni jinai.
-
Russia: Kuna wajibu kwa jamii ya kimataifa kuungana kukabiliana na jinai za Marekani
Nov 03, 2022 06:57Naibu wa Mkuu wa Timu ya Russia katika Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema, Marekani lazima ibebe lawama za jinai zake duniani na ameitaka jamii ya kimataifa kuungana kukabiliana na jinai hizo za Washington.
-
Associated Press: Marekani inatumia dola milioni mbili kwa mwezi kuwalinda wapangaji wa mauaji ya Qassem Soleimani
Mar 14, 2022 02:57Kwa mujibu wa tangazo la Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, dola milioni 2 hutumika kwa mwezi kutoka kwenye mifuko ya walipakodi nchini Marekani kuwalinda wanasiasa wawili wa Republican wenye msimamo mkali wa utawala wa Donald Trump na wahusika wa mauaji ya Kamanda Qassem Soleimani.
-
Brigedia Jenerali Shekarchi: Marekani ni mfadhili mkuu wa ugaidi, chanzo cha ukosefu wa usalama duniani kote
Jan 11, 2022 14:16Msemaji wa Jeshi la Iran ameitaja Marekani kuwa nchi inayoongoza kwa kufadhili ugaidi duniani na kusema Washington ndiyo chanzo cha ukosefu wa usalama kote duniani.
-
Brigedia Jenerali Qaani: Wauaji wa Kamanda Soleimani hawatakuwa salama
Jan 05, 2022 07:45Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Wauaji wa Luteni Jenerali Qasem Soleimani walidhani kuwa wameshinda kwa kumuua, lakini hawakujua kwamba hawatakuwa salama.
-
Nasrullah: Kupuuza uwepo wa US nchini Iraq, ni sawa na kumuua tena shahidi Soleimani
Jan 04, 2022 07:56Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kitendo cha kupuuza uwepo wa vikosi vamizi vya Marekani nchini Iraq, ni sawa na kuuawa shahidi kwa mara ya pili Luteni Jenerali Qasem Soleimani, aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
-
Kongamano la kumuenzi Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Mohandes lafanyika Tunisia
Dec 30, 2021 08:17Kundi la vyama vya siasa na asasi za kiraia nchini Tunisia zimefanya kongamano kwa mnasaba wa mwaka wa pili wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al-Muhandis, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha Hashd al Sha'abi.