Nov 03, 2022 06:57 UTC
  • Russia: Kuna wajibu kwa jamii ya kimataifa kuungana kukabiliana na jinai za Marekani

Naibu wa Mkuu wa Timu ya Russia katika Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa amesema, Marekani lazima ibebe lawama za jinai zake duniani na ameitaka jamii ya kimataifa kuungana kukabiliana na jinai hizo za Washington.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, VKonstantin Vorontsov amesema hayo na kusisitiza kuwa, Marekani haiwezi kukwepa adhabu ya jinai zake duniani. Amehoji kwa kusema: "Kwa nini jamii ya kimataifa hatuungani kuiadhibu Marekani kwa kumuua kigaidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, (Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH)?

Amesema, Marekani ilimuua Kamanda Soleimani akiwa uraiani tena kwenye safari ya kidiplomasia katika nchi ya tatu na akiwa mgeni rasmi wa serikali ya Iraq ambayo ni nchi huru na mwanachama wa Umoja wa Mataifa.

Luteni Jenerali Qassem Soleiman na Abu Mahdi al Muhandis waliouliwa kidhulma na wanajeshi magaidi wa Marekani mjini Baghdad Iraq

 

Luteni Jenerali Qassem Soleimani aliuliwa kigaidi na Marekani, alfajiri ya siku ya Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020 uraiani mjini Baghdad Iraq. Wanajeshi magaidi wa Marekani walifanya shambulio la anga kwa amri ya rais wa wakati huo wa Marekani, Donald Trump na kumuua kidhulma mpambanaji huyo mkubwa wa ugaidi duniani.

Afisa huyo wa Russia katika Umoja wa Mataifa pia amesema, si jambo la kushangaza kuona Uingereza, Marekani na Ufaransa zinapiga makelele na kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Russia tena kwa kutegemea taarifa za uongo. Ni nchi hizo hizo ndizo zilizoivamia mara mbili Syria katika miaka ya 2017 na 2018.

Amesema, nchi hizo za Magharibi ziliishambulia Syria kwa makombora kwa madai ya eti kuvunja taasisi za kijeshi za kemikali. Hivi sasa miaka mitano imepita na zimeshindwa kuiambia dunia majina ya taasisi hizo za mada za kemikali. "Je, miaka mitano haitoshi kugundua angalau majina ya hizo taasisi?" Amehoji.

Tags