-
Iran yatangaza utayari wa kuimarisha uhusiano wake na Tanzania
Sep 30, 2023 07:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian amesema, Jamhuri ya Kiislamu iko tayari kuimarisha uhusiano na maelewano ya pande mbili kati yake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-
Ghalibaf: Nchi za Afrika kwa Iran ni muhimu sana kama ilivyo kundi la BRICS
Sep 28, 2023 15:24Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema katika mazungumzo na wanaharakati na wabunge wa Afrika Kusini kwamba, Tehran inaamini kuwa, umuhimu wa nchi za Afrika hususan Afrika Kusini ni mkuubwa na ni sawa na umuhimu wa kundi la BRICS, kwa Iran.
-
Iran na Djibouti zakubaliana kufufua uhusiano wa kidiplomasia
Sep 23, 2023 04:08Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Djibouti wameafikiana juu ya kuhuisha uhusiano wa kidiplomasia wa Tehran na Asmara, kwa maslahi ya mataifa haya mawili.
-
Hilali Nyekundu ya Iran yatuma misaada ya kibinadamu Libya
Sep 17, 2023 04:39Mkuu wa Shirika la Hlilali Nyekundu la Iran (IRCS) amesema jumuiya hiyo imetuma tani 40 za misaada ya dharura nchini Libya, kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
-
Spika wa Bunge la Iran aelezea masikitiko yake kwa serikali na watu wa Libya baada ya mafuriko
Sep 14, 2023 02:55Katika ujumbe wake kwa Spika mwezake wa Bunge la Libya, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameelezea masikitiko yake kwa serikali na wananchi wa Libya kufuatia maafa makubwa ya roho na mali za watu yaliyosababishwa na mafuriko makubwa katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika
-
Iran yasikitishwa na zilzala iliyoua maelfu Morocco; kutuma nchini humo misaada ya kibinadamu
Sep 10, 2023 10:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu ipo tayari kutuma misaada ya kibinadamu nchini Morocco, kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoua maelfu ya watu.
-
Raisi: Mapambano ya nchi za Kiafrika dhidi ya ukoloni ni ishara ya mwamko na kuwa macho
Sep 04, 2023 14:06Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza kusimama kidete na mapambano ya nchi za Kiafrika dhidi ya ukoloni na ugaidi, na kuyataja kuwa ni ishara ya mwamko, kuwa macho na utambuzi sahihi wa mahitaji ya zama ya nchi hizo.
-
Raisi: Iran inajitahidi kuwa na uhusiano wa pande mbili uliokita mizizi katika kuheshimiana na mataifa ya Afrika
Aug 25, 2023 12:38Rais wa Iran Ebrahim Raisi anasema Tehran inataka kuwa na uhusiano na nchi za Kiafrika kwa kuzingatia msingi wa kuheshimiana na kufaidika, kinyume cha mataifa ya Magharibi ambayo yanataka tu kupora maliasili na utajiri wa Afrika.
-
Rais Ibrahim Raisi: Iran iko tayari kushirikiana na Tanzania katika nyuga mbalimbali
Aug 25, 2023 03:10Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza utayarifu wa Iran wa kushirikiana na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nyanja mbalimbali kama za kutoa huduma za uhandisi wa kiufundi, ujenzi wa mabwawa, mitambo ya kuzalisha umeme, kilimo na viwanda.
-
Rais wa Iran awasili Afrika Kusini kushiriki mkutano wa kilele wa BRICS
Aug 24, 2023 07:53Rais Ebrahim Raisi wa Iran amewasili Pretoria, mji mkuu wa kiutawala wa Afrika Kusini, alikoenda kushiriki mkutano wa kilele wa Jumuiya ya BRICS.