Apr 30, 2024 07:21 UTC

Watu watatu wameuawa katika ufyatuaj risasi uliotokea katika jimbo la North Carolina nchini Marekani.

Marekani, ambayo ni nchi iliyo na silaha nyingi zaidi ulimwenguni kote, kila wakati hushuhudia matukio ya ufyatuaji risasi dhidi ya makundi ya watu.

Uhuru wa kununua na kuuza na kubeba silaha nchini Marekani husababisha vurugu za utumiaji silaha na ufyatuaji risasi nchini kote, unaoteketeza roho za watu kila siku.

Zikilinganishwa takwimu za machafuko yanayotokana na utumiaji silaha kati ya Marekani na nchi nyingine duniani kote, nchi hiyo inaonekana kuwa na hali ya kipekee.

Kulingana na shirika la habari la IRNA, Johnny Jennings, Mkuu wa Polisi ya mji wa Shalott katika jimbo la North Carolina amesema, maafisa watatu wa polisi ya mji huo wameuawa kwa kupigwa risasi katika tukio la ufyatuaji risasi lililotokea katika jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Jennings, askari wa nne aliyepigwa risasi katika tukio hilo la ufyatuaji risasi alipelekwa hospitalini na hali yake imeripotiwa kuwa mbaya.

Mkuu huyo wa Polisi ya Shallot amefafanua zaidi na kusema kuwa, ufyatuaji risasi ulitokea wakati maafisa wa Polisi walipokwenda kutekeleza agizo la kumkamata mshukiwa mahali anapoishi.

Wakati wa ufyatulianaji wa risasi, mbali na mshukiwa mkuu aliyepigwa risasi na kuuawa na maafisa wa polisi, washukiwa wengine wawili pia walikamatwa ndani ya nyumba zilikofyatuliwa risasi na kuwaua askari polisi na wamepelekwa Idara ya Polisi ya Shalot kwa ajili ya kuhojiwa.

Shirika la Hifadhi za Matukio ya Ukatili wa Utumiaji Silaha nchini Marekani la (GVA) lilitangaza hapo kabla kwamba mnamo mwaka 2023, zaidi ya watu 42,000 waliuawa kwa silaha moto na baridi nchini humo.

 

Tags