Takriban wakimbizi elfu kumi wameaga dunia katika mpaka wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i111790-takriban_wakimbizi_elfu_kumi_wameaga_dunia_katika_mpaka_wa_marekani
Karibu wakimbizi na wahajiri elfu kumi wameaga dunia katika mpaka wa Marekani.
(last modified 2024-05-15T08:26:22+00:00 )
May 15, 2024 08:26 UTC
  • Takriban wakimbizi elfu kumi wameaga dunia katika mpaka wa Marekani

Karibu wakimbizi na wahajiri elfu kumi wameaga dunia katika mpaka wa Marekani.

Mpaka wa pamoja kati ya Marekani na Mexico umekabiliwa na mgogoro mkubwa wa vifo katika miaka ya hivi karibuni kufuatia sera kali za uhamiaji za Marekani.

Takwimu zinaonyesha kuwa, idadi ya wahamiaji waliofariki dunia katika mpaka wa Marekani mwaka 2022 ilivunja rekodi; ambapo katika mwaka huo, mabaki ya miili ya watu 895 yaligunduliwa upande wa Marekani wa mpaka wa nchi hiyo na Mexico. 

Wahamiaji kutoka Mexico kuelekea Marekani 

Kuzidi kugunduliwa mabaki ya miili ya wahamiaji, hasa katika mpaka wa jimbo la Texas la Marekani na Mexico, kumezidisha wasiwasi kuhusu ya majanga ya haki za binadamu. 

Kwa mujibu wa ripoti kuhusu vifo vya wahamiaji katika mpaka wa Marekani, kati ya mwaka 1998 na 2022, zaidi ya watu 9,500 walipoteza maisha upande wa Marekani katika mpaka wa nchi hiyo na Mexico, na weledi wa mambo wanaamini kwamba idadi hii tajwa ni ndogo kulinganisha na idadi halisi ya wahanga. Joto kali na kuzama majini ni miongoni mwa sababu zinazotajwa kusababisha vifo hivyo vya wahajiri.