Jan 05, 2022 07:45 UTC
  • Brigedia Jenerali Qaani: Wauaji wa Kamanda Soleimani hawatakuwa salama

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: Wauaji wa Luteni Jenerali Qasem Soleimani walidhani kuwa wameshinda kwa kumuua, lakini hawakujua kwamba hawatakuwa salama.

Brigedia Jenerali Ismail Qaani amesema: "Trump, mtenda jinai na wenzake wanajulikana na wa siri kama Pompeo tunawajua vizuri; wako chini ya darubini ya watu wote huru duniani na hawatakuwa salama."

Brigedia Jenerali Qaani amesema, kuondoka Wamarekani nchini Iraq ni sehemu ya mipango ya Iran na kwamba fedheha zaidi ya kuondoka huko ni kufukuzwa Wamarekani na kwamba Wairaqi na kambi ya muqawama na mapambano hawatastahamili askari elfu mbili wa nchi hiyo ambao bado wako Iraq. 

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ameongeza kuwa, Iran italipiza kisasi cha mauaji ya Shahidi Qasem Soleimani kwa kutumia mbinu na mtindo wake na si kwa mtindo wa watenda jinai duniani. 

Kufuatia jinai hiyo iliyofanwya na ndege za kivita za Marekani kwa amri ya moja kwa moja ya rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump, mnamo Januari 8 mwaka 2020, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu lilichukua hatua ya kulipiza kisasi kwa kuvurumisha makombora kadhaa dhidi ya kambi ya wanajeshi wa Marekani ya Ain al Assad nchin Iraq na kuisawazisha kabisa na ardhi. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza kuwa bado haijamaliza kulipiza kisasi cha mauaji ya Shahidi Soleimani.

Tags