Somalia: Uingiliaji kati wa Israel ni changamoto kwa bara zima la Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i136364-somalia_uingiliaji_kati_wa_israel_ni_changamoto_kwa_bara_zima_la_afrika
Rais wa Somalia amekosoa vikali uingiliaji kati wa utawala wa kizayuni Israel katika masuala ya ndani ya nchi hiyo na kueleza kwamba, hatua hiyo ya Wazayuni ni changamoto kwa bara zima la Afrika.
(last modified 2026-02-07T11:42:00+00:00 )
Feb 07, 2026 11:42 UTC
  • Somalia: Uingiliaji kati wa Israel ni changamoto kwa bara zima la Afrika
    Somalia: Uingiliaji kati wa Israel ni changamoto kwa bara zima la Afrika

Rais wa Somalia amekosoa vikali uingiliaji kati wa utawala wa kizayuni Israel katika masuala ya ndani ya nchi hiyo na kueleza kwamba, hatua hiyo ya Wazayuni ni changamoto kwa bara zima la Afrika.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, likinukuu Al Jazeera, Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia amesisitiza: "Dunia lazima iamke na kusimama dhidi ya wale wanaokiuka sheria za kimataifa."

Ameongeza kwa kusema: " Sisi nchini Somalia tunapambana na wapiganaji wa makundi ya kigaidi ya al-Qaeda na Daesh. Mvutano wa kikanda na misimamo inayovuruga utulivu kama vile uingiliaji kati wa utawala wa kizayuni wa Israel unavuruga utulivu wa kikanda."

Kadhalika Rais wa Somalia amesema: "Uingiliaji kati wa Israel nchini Somalia ni kinyume cha sheria. Uingiliaji kati huu hautishii Somalia tu, bali pia ni changamoto kwa bara zima la Afrika."

Amesema: "Tunaonya vikali dhidi ya jaribio lolote la kubadilisha mfumo wa sasa wa kimataifa na hatupaswi kurudi kwenye mantiki ya nguvu na mabavu. Kuhusu suala la Palestina, pia nasema kwamba, ni lazima kuweko suluhisho la kudumu na jumuishi ambalo limejengeka juu ya msingi wa suluhisho la mataifa mawili.

Ikuumbukwe kuwa, hivi karibuni utawala ghasibu wa Israel ulitangaza kutambua jimbo lililojitenga na Somalia la Somaliland kama nchi huru uamuzi ambao umeendelea kukosolewa na kulaaniwa kimataifa.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991 kufuatia vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe lakini haijawahi kutambuliwa rasmi na nchi yoyote mwanachama wa Umoja wa Mataifa.