Mkataba wa Maelewano na Iran: Mwisho wa nguvu ya Dola la Marekani
Tucker Carlson, mtangazaji na mchambuzi mashuhuri wa Marekani, amesema katika taarifa kuhusu makubaliano ya hivi karibuni kati ya Iran na Marekani kwamba makubaliano hayo yamemaliza kikamilifu nguvu, kiburi, majigambo na ubabe wa Marekani katika ngazi ya kimataifa na kuipelekea ikiri rasmi hadharani kwamba Iran ni mchezaji muhimu mwenye maamuzi huru, na kwamba hilo pekee limebadilisha kila kitu katika mtazamo wa kisiasa na kijeshi.
Mchambuzi huyo mashuhuri wa masuala ya kisiasa wa nchini Marekani anasema makubaliano hayo, yameonyesha kuwa licha ya kuwa na jeshi bora, kubwa na la gharama kubwa zaidi duniani, lakini limeshindwa kushinikiza na kulazimisha matakwa yake dhidi ya Iran, ambayo ni nchi ya 34 kwa uchumi mkubwa duniani. Amesema kama "Mgogoro wa Suez mnamo 1956" ulivyoashiria kupungua kwa nguvu na ushawishi wa Dola la Uingereza, makubaliano haya pia yanaonyesha wazi kupungua kwa nguvu na ufalme wa Marekani duniani.
Amemalizia kwa kusema kuwa utekelezaji wa mkataba wa maelewano wa Islamabad utaimarisha nguvu ya kieneo ya Iran na, kwa upande wa pili, kudhoofisha uwepo na ushawishi wa Marekani katika Asia Magharibi.