Abbas Araqchi: Mazungumzo ya Muscat yamekuwa na mwanzo mzuri
-
Abbas Araqchi: Mazungumzo ya Muscat yamekuwa na mwanzo mzuri
Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya nje wa Iran amesema kuwa, mazungumzo ya nyuklia yasiyo ya moja kwa moja na Marekani huko Muscat Oman yamekuwa na mwanzo mzuri, huku hatua za baadaye zikitegemea mashauriano katika miji mikuu.
Wawakilishi wa Iran na Marekani leo wamefanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja mjini Muscat, Oman kuhusu mpango wa nyuklia wa amani wa Iran na kuondolewa vikwazo vya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Seyed Abbas Araghchi amesema kuwa, wamefanya majadiliano marefu na mazito yasiyo ya moja kwa moja kuanzia asubuhi hadi jioni, huku kukiwa na mazungumzo kadhaa. Alisisitiza kwamba Iran ilielezea waziwazi mitazamo yake, wasiwasi, na haki na maslahi ya watu wa Iran "katika mazingira chanya sana."
Araghchi amesisitiza kwamba ingawa kuna makubaliano kuhusu kuendelea kwa mchakato huo kimsingi, maamuzi kuhusu muda na taratibu zinahitaji mashauriano katika miji mikuu husika. Alibainisha kuwa kujenga upya uaminifu bado ni changamoto kubwa lakini akasema majadiliano yalishughulikia suala hili moja kwa moja na kwa njia ya kujenga.
Mazungumzo ya nyuklia na kuondolewa vikwazo Iran kati ya Tehran na Washington yamefanyika leo, Ijumaa, Februari 7, huko Muscat, mji mkuu wa Oman, kwa upatanishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo.
Ajenda kuu ya mazungumzo hayo yasiyo ya moja kwa moja ni faili la la nyuklia la Iran na kuondolewa vikwazo taifa hili vilivyowekwa na Marekani.
Oman imekuwa na jukumu kubwa kama mpatanishi kati ya nchi za kikanda katika miaka ya hivi karibuni, na mazungumzo ya leo inaonekana kama mwendelezo wa mpango wa kidiplomasia wa nchi hii wa kupunguza mvutano katika eneo hilo.