Abbas Araghchi atoa wito wa suluhisho la kiadilifu kwa kadhia ya Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136370-abbas_araghchi_atoa_wito_wa_suluhisho_la_kiadilifu_kwa_kadhia_ya_palestina
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa wito wa kuwepo suluhisho la kiadilifu na endelevu katika kutatua kadhia ya Palestina.
(last modified 2026-02-07T12:09:50+00:00 )
Feb 07, 2026 12:09 UTC
  • Abbas Araghchi atoa wito wa suluhisho la kiadilifu kwa kadhia ya Palestina
    Abbas Araghchi atoa wito wa suluhisho la kiadilifu kwa kadhia ya Palestina

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametoa wito wa kuwepo suluhisho la kiadilifu na endelevu katika kutatua kadhia ya Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema hayo leo katika mji mkuu wa Qatar Doha katika hotuba yake katika Jukwaa la 17 la Al Jazeera lenye anuani "Kadhia ya Palestina na Uwiano wa Kikanda Katika Ulimwengu wa Pande Nyingi," na kusisitiza kwamba, Palestina si daghadagha na hangaiko la kikanda au la kibinadamu tu, bali ni jiwe la msingi la usalama endelevu katika Asia Magharibi na mtihani wa kufungamana jamii ya kimataifa na sheria za kimataifa.

Araghchi ameelezea hali inayoendelea Gaza kama zaidi ya mzozo wa kijeshi wa kawaida, akisisitiza mauaji ya halaiki ya raia na uharibifu wa miundombinu muhimu kama ukiukwaji wa sheria za kimataifa na kielelezo na mfano wa wazi wa mauaji ya kimbari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameonya kwamba, kinga inayoendelea ya Israel dhidi ya uwajibikaji inadhoofisha misingi yya kisheria za kimataifa na inahatarisha kuchukua nafasi ya utawala wa sheria kuchukuliwa na vitendo vya utumiaji mabavu, na kusababisha vitisho vikubwa kwa amani na utulivu Palestina.

Amesisitiza kwamba suluhisho lolote la kiadilifu na endelevu kuhusu Palestina lazima lijumuishe kukomesha uvamizi, haki ya kurejea wakimbizi wa Palestina, na kuanzisha taifa huru na lenye umoja la Palestina mji mkuu wake ukiwa Baytul-Muqaddas.

Akizungumzia upande wa kikanda, Araghchi amebainisha kuwa vitendo vya utawala haramu wa Israel ikiwa ni pamoja na ukiukaji wa uhuru na mamlaka ya kujitawala nchi, mauaji yaliyolenga maafisa, na upanuzi wa shughuli za kijeshi bila hatua za kimataifa vimeongeza ukosefu wa usalama katika eneo lote la Asia Magharibi.