Meja Jenerali Mousavi: Tumeimarisha uwezo wa makombora yetu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i136308-meja_jenerali_mousavi_tumeimarisha_uwezo_wa_makombora_yetu
Afisa mwandamizi wa Jeshi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imeimarisha mifumo yake ya kujilinda kwa kuboresha makombora ya balestiki yaliyotengenezwa ndani ya nchi.
(last modified 2026-02-06T02:56:48+00:00 )
Feb 06, 2026 02:56 UTC
  • Meja Jenerali Mousavi: Tumeimarisha uwezo wa makombora yetu

Afisa mwandamizi wa Jeshi wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu imeimarisha mifumo yake ya kujilinda kwa kuboresha makombora ya balestiki yaliyotengenezwa ndani ya nchi.

Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi, Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran amesema hayo wakati wa ziara yake katika mji wa makombora wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

"Kwa kuboresha makombora yake ya balestiki katika nyanja zote za kiufundi, Iran imeweza kuimarisha nguvu yake ya kujilinda," amesema wakati wa ziara hiyo, akiwa pamoja na Brigedia Jenerali Majid Mousavi, Kamanda wa Kikosi cha Anga cha IRGC.

Aidha Mkuu wa Majeshi ya Iran ameelezea utayarifu wa vikosi vya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu katika kukabiliana na kitendo chochote cha uchokozi kutoka kwa maadui zake.

"Kufuatia vita vya siku 12, tumebadilisha doktriji yetu ya kijeshi kutoka kujihami hadi kushambulia kwa kupitisha sera ya vita visivyo na mlingano na [kuongeza utayari wa] kukabiliana vikali na maadui," Meja Jenerali Mousavi amesema.

Alikuwa akirejelea mashambulizi ya kichokozi na haramu ya Marekani na Israel dhidi ya Iran ambayo yaliua shahidi watu wasiopungua 1,064 mwezi Juni mwaka uliopita.

Mapema wiki hii, Jenerali Mousavi alionya kwamba, makosa yoyote yatakayofanywa na maadui wa Jamhuri ya Kiislamu yatakabiliwa na jibu la "haraka" na "zito."

Vikosi vya Jeshi la Iran vimejiandaa kujibu chokochoko za maadui kwa nguvu, alisisitiza na kuongeza kuwa,"Tunafikiria ushindi tu. Hatuogopi nguvu bandia ya adui, na tuko tayari kikamilifu kwa mapambano na kutoa pigo la kulipiza kisasi."