-
Kamisheni ya Bunge: Marekani itarajie kisasi kikali kwa hatua yake ya kumuua Qassim Soleimani
Jan 04, 2020 09:44Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Siasa za Kigeni katika Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imesisitiza kuwa, Marekani mtenda jinai isubirie kisasi kikali dhidi yake kutokana na hatua yake ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH).
-
Umati mkubwa wausindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani mjini Baghdad
Jan 04, 2020 09:12Umati mkubwa wa watu umejitokeza leo katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad kushiriki shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa shahidi Qassim Soleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliyeuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad.
-
Rouhani: Jina la Qassem Soleimani litabakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani
Jan 04, 2020 04:46Rais Hassan Rouhani amesema: Jina la Luteni Jenerali Qassem Soleimani litaheshimika na kubakia milele katika historia ya taifa la Iran na wapigania uhuru duniani.
-
Kumuua shahidi Kamanda Soleimani, kosa kubwa mno la kiistratijia la Marekani
Jan 04, 2020 04:06Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetoa tamko maalumu kufuatia jinai ya Marekani ya kumuua shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH. Taarifa hiyo ya jana Ijumaa ilitolewa baada ya kikao cha dharura cha baraza hilo ambacho kilichunguza pembe mbalimbali za tukio hilo la kuchukua maamuzi yanayofaa.
-
Balozi wa Iran UN: Jibu la mauaji ya kigaidi ya Jenerali Soleimani litakuwa la hatua ya kijeshi
Jan 04, 2020 03:46Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amesema, jibu la mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Soleimani yaliyofanywa na Marekani bila shaka litakuwa la hatua ya kijeshi.
-
Amiri Jeshi Mkuu Iran amteua kamanda mpya wa kikosi cha Quds cha IRGC
Jan 03, 2020 23:20Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Iran amemteua Brigedia Jenerali Esmail Qaani kuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).
-
IRGC yaahidi hatua kali ya kulipiza kisasi baada ya kuuawa shahidi Soleimani
Jan 03, 2020 23:19Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu limetuma salamu za rambirambi kufuatia kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassem Suleimani Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na mashahidi wengine katika jinai ya Marekani Ijumaa asubuhi mjini Baghdad na kusisitiza kuhusu kulipiza kisasi kufuatia jinai hiyo.
-
Kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Solaimani; ahadi ya kweli iliyotimia
Jan 03, 2020 23:09Meja Jenerali, Qassim Solaimani, Meja Jenerali shahidi Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH), aliuawa shahidi usiku wa kuamkia jana Ijumaa katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.
-
SAUTI, Fadhil Al-Nusr Muhadhiri Chuo Kikuu Tanzania: Qassem Soleimani hakuwa tu kamanda wa kijeshi bali alikuwa mlezi mkubwa wa kiroho
Jan 03, 2020 12:42Dunia imeendelea kutoa radiamali yake kutokana na kuuawa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani aliyeuawa shahidi kigaidi na helikopta ya kijeshi ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mjini Baghdad nchini Iraq mapema leo asubuhi.
-
SAUTI, Mansour Amr wa Kongo DR: Qassem Soleimani alikuwa zaidi ya makamanda duniani, hakusema kwa maneno bali kwa vitendo
Jan 03, 2020 11:16Dunia imegubikwa na huzuni kubwa ya kuuawa Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani aliyeuawa shahidi kigaidi na helikopta ya kijeshi ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa mjini Baghdad nchini Iraq mapema leo asubuhi.