-
Khatibu wa Sala ya Ijumaa: Wamarekani katu hawatapata amani
Jan 03, 2020 09:07Khatibu wa Sala ya Ijumaa iliyoswaliwa leo hapa mjini Tehran ameashiria juu ya kuuliwa shahidi Meja Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kusisitiza kuwa, Wamarekani katu hawataonja tena ladha ya amani popote duniani kufuatia ukatili huo.
-
Wairani waandamana kote nchini kuomboleza mauaji ya Jen. Soleimani
Jan 03, 2020 09:02Wananchi wa Iran katika mikoa na miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Tehran wamemiminika mabarabarani baada ya Sala ya Ijumaa kushiriki maandamano ya kuomboleza na kulaani mauaji ya kamanda wa ngazi za juu wa Jeshi la Iran.
-
Kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Solaimani; mfano wa wazi wa jinai za kivita za Marekani
Jan 03, 2020 08:23Meja Jenerali Qassim Solaimani, Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) na Abu Mahdi al Muhandes, Naibu Mkuu wa Kikosi cha Kujitolea cha Wananchi wa Iraq cha al-Hashdul al-Shaabi, wameuawa shahidi usiku wa kuamkia Ijumaa ya leo katika shambulio la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad mji mkuu wa Iraq.
-
Msemaji wa jeshi la SEPAH: Furaha ya Marekani na Israel itageuka kuwa maombolezo
Jan 03, 2020 04:51Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH, huku akiomboleza kuuawa shahidi Meja Jenerali Qassim Soleimani, Kamanda wa kikosi cha Quds cha jeshi hilo amesisitiza kwamba furaha ya muda mfupi ya Wamarekani na Wazayuni itageuka kuwa maombolezo hivi karibuni.
-
Mkuu wa Mahakama za Iran na Spika wa Bunge: Iran italipiza kisasi cha damu ya Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 04:40Mkuu wa Idara ya Vyombo vya Mahakama nchini Iran na Spika wa Majlisi ya Ushari ya Kiislamu (Bunge) hapa nchini wamesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu italipiza kisasi cha damu ya Shahidi Qassem Soleimani aliyeuawa mapema leo katika shambulizi la Marekani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
-
Rais Rouhani: Kuuliwa shahidi Soleimani kutazidisha azma ya Iran ya kupambana na ubeberu wa Marekani
Jan 03, 2020 03:52Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, kuuliwa shahidi Meja Jenerali Qassem Solaimani aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi al Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) kutazidisha mara dufu azma ya Iran na mataifa mengine huru ya kusimama kidete kupambana na ubeberu wa Marekani na kulinda thamani na maadili ya Kiislamu.
-
Kiongozi Muadhamu: Kisasi kikali kinawasubiri waliomuua shahidi Jenerali Soleimani
Jan 03, 2020 03:21Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ametuma salamu za rambirambi kutokana na kuuliwa shahidi Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Meja Jenerali Qassem Solaimani na kusema kuwa: Kisasi kikali kinawasubiri watenda jinai ambao mikono yao michafu imemwaga damu yake na mashahidi wengine katika shambulizi la usiku wa kuamkia leo.
-
Jenerali Qassem Soleimani na Abu Mahdi al Muhandes wauawa shahidi na helikopta ya Marekani, uwanja wa ndege wa Baghdad
Jan 02, 2020 23:58Duru za habari zinaripoti kuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) Meja Jenerali Qassem Solaimani na naibu mkuu wa kikosi cha kujitolea cha wananchi wa Iraq, al Hasdul Shaabi, Abu Mahdi al Muhandes wameuawa shahidi mapema leo Ijumaa katika shambulizi la roketi lililofyatuliwa na helikopta ya Marekani katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad nchini Iraq.
-
Meja Jenerali Mousavi: Iran itatoa jibu kali na la haraka ikichokozwa
Jan 02, 2020 23:22Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema vikosi vya Jeshi la Iran viko tayari kutoa jibu kali na la haraka kwa aina yoyote ya vitisho na chokochoko za adui.
-
IRGC: Iran ya Kiislamu imefikia kilele cha nguvu na uwezo mkubwa
Jan 02, 2020 23:21Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran (IRGC) sambamba na kuashiria vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya raia wa nchi hii amesema kuwa, hii leo Iran ya Kiislamu iko kwenye kilele cha nguvu na uwezo mkubwa.